Friday 5 July 2013

Kundi Jipya la Muziki laja Jijini, kutambulika kwa Jina la Ndege Watatu.

PICT1
Kutoka kushoto ni Paulyne Zongo, Khadija Mnoga (Kimobitel) na Joan Matovolwa. Wanamuziki hao watatu na wakongwe nchini ndio wanaounda kundi hilo litajulikana kwa jina la NDEGE 3.
PICT2
Kundi la Ndege 3 linaloundwa na wanamuziki wakongwe katika Tasnia ya muziki wa dansi na kizazi kipya Joan matovolwa, Khadija Mnoga (Kimobitel) na Paulyne Zongo, hivi karibuni limeshatoa kibao chake kinachokwenda kwa jina la MISUKOSUKO YA MAPENZI ambacho redio kadhaa nchini zimeanza kukirusha.
MISUKOSUKO YA MAPENZI ni nyimbo ambayo imetungwa kwa umahiri wa hali ya juu, na kuonyesha viwango vya juu katika uimbaji na utunzi.
Kwa sasa Joan Matovolwa na Paulyne Zongo ni wanamuziki huru wakati Khadija Mnoga (Kimobitel) ni mwanamuziki anayeimba katika bendi ya Extra Bongo inayoongozwa na Camarade Ally Choki.
CHANZO: Mo blog

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...