Saturday 6 July 2013

Mamlaka ya Elimu Tanzania yasaidia Kupanua Wigo wa Elimu Jumuishi nchini.

Msemaji wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA),Sylvia Lupembe (Katikati), akiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari 9MAELEZO), AQssah Mwambene (Kushoto), na Mkurugenzi saidizi wa idara hiyo anayeshughulikia uratibu wa maweasiliano serikalini, Zamaradi Kawawa, akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana. Idara hiyo imeanzisha utaratibu ujulikanao kama (Meet The Press), ambao utawataka wasemaji wa idara za serikali kukutana na waandishi wa habari kila siku za kazi makao makuu ya idara hiyo, ili kuzungumzia mambo mbalimbali yahusuyo maeneo yao. Aliserma Assah. (Picha na Khalfan Said)

Meneja Habari, Elimu na Mawasiliano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Sylvia Lupembe (katikati) akifafanua mipango ya kupanua wigo wa elimu nchini kwa waandishi wa habari kwenye mkutano uliofanyika Maelezo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Assah Mwambene na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Maelezo Zamaradi Kawawa.
PIX 2
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Assah Mwambene (kushoto) akisisitiza jambo kwa Waandishi wa Habari waliohudhuria Mkutano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) katika ukumbi wa Habari Maelezo leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Meneja Habari Elimu na Mawasiliano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania, Sylvia Lupembe na kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari, Zamaradi Kawawa. (PICHA NA KHALFAN SAID WA THE GUARDIAN).
VIDOKEZO
-Taasisi 119 katika ngazi za elimu ya Msingi, Sekondar,i Vyuo vya Ualimu na Vyuo Vikuu vimepata vifaa na kuboreshewa miundo mbinu kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum
-Wanafunzi wenye mahitaji maalum wapatao 3,114 wanufaika na ufadhili huo.
-Kujenga hosteli 30 za wasichana katika shule za sekondari za kata.
Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) katika kuendelea kutoa ruzuku kwa taasisi za elimu kwa lengo la kuongeza ubora katika utoaji elimu, pamoja na miradi mingine imelenga kupanua wigo wa elimu jumuishi kwa ngazi mbalimbali za elimu nchini.


‘Elimu jumuishi’ ni ile inayotambua mahitaji tofauti ya kujifunza ya wanafunzi ili kuhakikisha wanawekewa mazingira bora yenye kukidhi mahitaji yao. Tanzania inatekeleza utaratibu huu baada ya kuridhiria mpango wa utekelezaji Elimu Maalum wa Salamanca mwaka 1994. Mpango  unasisitiza kuwa watoto wote wajifunze kwa pamoja kadri inavyowezekana, bila kujali tofauti za kijiografia, maumbile, jinsia, uwezo wa kiakili.  Changamoto ni kuhahakikisha kuna vifaa vya kutosha kukidhi mahitaji hayo.
Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) imesaidia kuongeza wigo wa utekelezaji wa mpango huu kwa kutoa vifaa mbalimbali vya kujifunzia na kufundishia wanafunzi wenye mahitaji maalum na vifaa saidizi.  Jumla ya  taasisi 119 tayari zimeshafaidika na wanafunzi 3,114 wamenufaika na vifaa hivyo.
Aidha misaada iliyotolewa ni pamoja na:-
(a)       vifaa saidizi kwa wanafunzi wenye ulemavu kama fimbo nyeupe, vifaa vya kuongeza usikizi, miwani mafuta maalum kwa wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi
(b)        vifaa vya kujifunza na kufundishia kama mashine za maandishi ya nukta nundu, vifaa vya TEKNOHAMA kama kompyuta maalum kwa wasioona, mashine ya kutoa machapisho kwa nukta nundu, vitabu vya kiada vya lugha za alama. 
(c)        Ukarabati au ujenzi wa miundo mbinu kama madarasa, mabweni ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi wenye ulemavu;
(d)        Kuboresha mazingira ya vyuo vya mafunzo ya walimu wa elimu maalum.
Kati ya mwaka 2011 hadi 2013TZS 1,000,940,140.00 zimetumika kugharamia  ununuzi wa vifaa hivyo na kuvisambaza. Baadhi ya taasisi zilizonufaika ni pamoja na Chuo cha ualimu patandi- Arusha , Buigiri- Dodoma , Njia panda- Kilimanjaro, Katesh- manyara na Maisaka Bariadi.  
MPANGO ENDELEVU
 Utoaji wa vifaa saidizi na vya kufundishia na kujifunzia kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum,  bado ni kipaumbele TEA na katika mwaka fedha 2012/13 tumetafuta wafadhili ili kwa pamoja tuweze kutoa msaada wa vifaa vya TEKNOHAMA kwa ajili ya wanafunzi wenye ulemavu katika Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania na Chuo cha ualimu Patandi. Mpango huu utasaidia kuongeza idadi ya waalimu wenye ujuzi wa elimu maalum.
Aidha kwa upande mwingine, Mamlaka pia imejikita katika kujenga hosteli za wasichana katika shule za sekondari za kata.   Jumla ya hosteli 30 zinatarajiwa kujengwa katika shule 8 kwa awamu ya kwanza kuanzia mwaka huu wa fedha . Hosteli hizo zitahudumia wanafunzi wa kike 1,504.   Mradi huu utagharimu jumla ya TZS bllioni 2.3.  na utawezesha kuongeza uwiano wa kijinsia katika shule za sekondari.
MAMLAKA YA ELIMU TANZANIA (TEA)
TEA ina jukumu la kuhamasisha jamii kushiriki kuchangia maendeleo ya sekta ya elimu kupitia Mfuko wa Elimu na kufadhili miradi ya elimu. Tunatambua jukumu la kuhakikisha upatikanaji wa Elimu bora letu sote kila mmoja wetu kwa nafasi yake. Watanzania mmoja moja, makampuni, mashirika tunaomba muendelee kuchangia Mfuko wa Elimu ili kuisadia serikali kutimiza lengo la utoaji elimu bora kwa kila mtanzania .
Bibi . Sylvia  Lupembe
Meneja Habari , Elimu na Mawasiliano, Mamlaka ya Elimu Tanzania  

5 Julai 2013
 kwa taarifa zaidi wasiliana na : Sylvia Lupembe Gunze, simu +255 2775468/68 au 0784664433; au tuma barua pepe kwenda : info@ tea.or.tz au slupembe@tea.or.tz Taarifa hii pia inapatikana katika tovuti ya TEA www.tea.or.tz

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...