Monday 1 July 2013

MAREKANI KUFUNGUA UKURASA MPYA KATIKA UWEKEZAJI

3

Rais wa Marekani Barack Obama akiwahutubia wafanyabiashara leo(jana) jijini Dar es salaam juu ya mpango wa Nchi yake wa kufungua milango ya ushirikiano na uwekezaji kwa Nchi za Afrika Mashariki katika sekta mbalimbali na hivyo kuongeza kiwango cha bidhaa ya Afrika Mashariki zinazoingia nchini Marekani.
4Rais wa Marekani Barack Obama akiwa katika mkutano jana (leo) jijini Dar es salaam wa kujadiliana na watendaji wakuu(CEO) wa Makampuni mbalimbali yaliyowekeza Afrika juu ya kuimarisha fursa za ushirikiano kati ya Marekani na Afrika katika uwekezaji kwenye sekta mbalimbali za maendeleo.
(Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dar es salaam)
………………………………………………
Na Eleuteri Mangi—MAELEZO—Dar es salaam
Serikali ya Marekani imeahidi kufungua ukurasa mpya kwa Nchi za Afrika Mashariki kwa kuongeza uwekezaji katika sekta mbalimbali ili kuinua uchumi wan chi hizo.


Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dar es salaam na Rais Barack Obama kwenye hotuba yake kwa wafanyabiashara wakati wa ziara yake ya siku mbili nchini Tanzania.
Alisema kuwa hatua hiyo inalenga kuongeza kiwango cha bidhaa kutoka Nchi za afrika Mashariki kuingia nchini Marekani na hivyo kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na kiuchumi kwa manufaa ya pande zote.
 “Sasa ni wakati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwekeza nchini Marekani  ili kuongeza mauzo yake nchini Marekani hadi ifike asilimia 40,” alisema Rais Obama.
Aliongeza kuwa pia ushirikiano huo unapaswa kuboresha utoaji wa mizigo katika bandari ya Dar  es salaam na Mombasa  kwenda nchi zisizo na bandari ili kuinua uchumi wa eneo hilo kwa kupunguza muda wa mizigo kukaa bandarini.
Akizungumzia hotuba ya Rais Obama Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye viwanda nchini (CTI) Felix Mosha alipongeza hotuba hiyo kwa kufungua ukurasa mpya kwa nchi za Afrika na Marekani kwa kuonyesha kuwa wakati wa kutegemea misaada umepitwa na wakati badala yake ni kushirikiana katika uwekezaji.
Katika mkutano huo kiasi cha wafanyabiashara 170 walihudhuria mkutano huo .

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...