Rais Barack Obama akigongesha glasi na mwenyeji wake rais Jakaya Kikwete wakati wa chakula cha usiku,jumatatu julai mosi.
Rais Barack Obama wa Marekani na mkewe Michelle wakiangalia ngoma za utamaduni pamoja na bendi ya polisi wakati wa dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa na mwenyeji wake Rais Jakaya Mrisho kikwete. Kushoto ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Serikali ya Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein. PICHA NA IKULU
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Rais Barak Obama wa Marekani kwa Mawaziri wakuu wastaafu pamoja na viongozi wengine wakati wa dhifa ya kitaifa aliyomwandalia mgeni huyo Jumatatu usiku Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na wageni wake Rais Barack Obama wa Marekani na mkewe Michelle wakati wa dhifa ya kitaifa aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Usiku. Kushoto ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein na Kulia ni Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda
No comments:
Post a Comment