Wednesday 3 July 2013

SEHEMU YA MAHOJIANO YA MSANII ELIZABETH MICHAEL(LULU) NA ZAMARADI



Nadhani Lulu kwa ushauri wa bure ungejaribu kutumia lugha moja kama ni kiswahili ongea kiswahili na kama ni kiingereza basi ongea kiingereza.Sio mambo ya yah,actually, maybe, it´s like,outcome...n.k.Haipendezi.
Ni busara uamue kufanya mahojiano kwa lugha ambayo una uwezo wa kuongea na si kuchanganyachanganya actually na may be na kuwapa taabu wengine katika kuelewa.Mimi si muumini wa kiswanglish na ninakipinga sana.Napenda tuikuze lugha yetu maana usipokuza chako kitakuzwa na nani?
Unaweza kuongea lugha yoyote uipendayo kwa mapenzi yako ila usichanganye changanye na lugha nyingine bila mpango.Labda kama neno unaloongea liwe limechukuliwa kutoka lugha nyingine hapo sawa. Kama unaongea kifaransa basi ongea hicho usiweke actally zako humo na kama unaongea kihispania basi ongea hicho na usiweke mayy be zako hizo.
 Kuchomekea maneno ya kiingereza  hakumaanishi kuwa wewe ni bab kubwa bali ni ULIMBUKENI.
Tembeeni muone jinsi wenzetu wanavyothamini lugha zao.Hakuna mambo ya yah wala actuaally.
Ujumbe huu si kwa Lulu tu bali wapo wengi wenye tabia hii.Lulu kama msanii wewe ni kioocha jamii hivyo unatakiwa kuielimisha jamii sasa kwa hizo actually sijui unatoa elimu gani hapo.
Nimekutana na watu wengi wa mataifa mbalimbali na sijaona mtu anaeongea lugha yake na kuchanganya na kingereza.Mfano sijaona mwarabu anaongea lugha yake na kuchanganya na kingereza au Mturuki anachanganya na kingereza,Mfini anachanganya na kingereza,Mswidi anachanganya na kingereza.AIBU ipo kwetu sisi tusiojiamni.
Mwalimu Nyerere alifanya jambo jema sana kutuunganisha kwa lugha moja,KISWAHILI.Sasa iweje tunamsaliti?Kiswahili ndiyo kimeimarisha umoja wetu watanzania sasa tukiendeleza hizi actually sijui tunaelekea wapi.
Lugha ndiyo utambulisho mkuu wa utamaduni na utaifa.Sasa kwa mtanzania kuchanganya Kiswahili na kiingereza tunajitambulishaje?
Ni hayo tu.

Anna
Stockholm,Sweden

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...