Monday 1 July 2013

WATU HAWA WANATAFUTWA NA JESHI LA POLISI KOKOTE WALIPO


Jeshi la Polisi linazo taarifa za kuaminika kuhusu watu hawa, wanaoonekana katika hizo picha hapo chini, ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vikubwa vya kihalifu hapa nchini na katika maeneo mbalimbali nje ya nchi yetu.

Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi wote wazalendo na wenye mapenzi mema na nchi yetu, kutoa taarifa za watu hawa popote watakapoonekana katika kituo chochote cha Polisi kilicho caribĂș, ili waweze kukamatwa na kufikishwa kwenye mkondo wa sheria.

Ndugu mwananchi, hata kama ni ndugu yako, usisite kutoa taarifa za watu hawa kwa sababu ni watu hatari sana. Zawadi nono itatolewa kwa yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa watu hao.

Kwa taarifa unaweza pia kupiga Makao Makuu ya Polisi kwa kutumia simu namba 0754 78 55 57.

Imetolewa na:- 
 Advera Senso - SSP 
 Msemaji wa Jeshi la Polisi(T)




CHANZO:Othman Michuzi

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...