Tuesday 8 September 2015

VIBIBI



Vipimo
2 kikombe Mchele                                                      
1 1/2 kikombeTui la nazi                                                 
1 KJ Mafuta                                                      
2 kjc Hamira                                                      
1 KJ Unga wa ngano                                           
Hiliki-Kulingana na matakwa yako                                                   
¾ au kikombe Sukari  

                                                     
FANYA HIVI
1·  Osha na roweka mchele usiku mzima ndani ya maji baridi.
2·  Mimina vifaa vyote isipokuwa sukari , ndani ya mashine ya kusagia (blender) na usage mpaka mchele uwe laini.
3·  Mimina ndani ya bakuli na ufunike.Weka mahali penye joto ili mchanganyiko ufure.
4·  Ukishafura , mimina sukari na changanya vizuri.Ongeza maziwa kidogo kama mchanganyiko ni mzito.
5·  Weka chuma kipate moto.
6·  Paka mafuta au samli kidogo kwenye chuma kisha mimina mchanganyiko kiasi kuunda duara na ufunike.
7·  Utazame ikishaiva upande mmoja , geuza upande wa pili mpaka iwe tayari.

8·  Endelea Mpaka umalize mchanganyiko wote; panga kwenye sahani na tayari kuliwa.

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...