Skip to main content

WASTARA AZIMIA NDANI YA GARI LAKE

Staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma akilia ndani ya gari lake.
Brighton Masalu
MASKINI! Staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma amezimia ndani ya gari, kisa kikiwa ni sakata la dada zake kuibiana mume, Amani linaweza kuandika.
Mkasa huo wa kusikitisha ulijiri mapema wiki hii, Kinondoni, Dar ambapo staa huyo alikuwa ameegesha gari lake pembeni mwa barabara.
Kabla ya kuzimia, Wastara aliliambia Amani kuwa, kitendo cha mdogo wao (mtoto wa mama yao mdogo), Janat kupora mume wa dada yake, Naima Juma (dada wa damu wa Wastara) aitwaye Masoud na kufunga naye ndoa kimyakimya, kimeipasua familia.


Akiwa amezimia ndani ya gari hilo.
Wakati mahojiano yakiendelea, ghafla Wastara alianza kuangua kilio na kulaani kitendo hicho akikiita cha kinyama.
“Kinachoniuma ni kitendo cha mama wa Janat, Jamila Salum kutamka kuwa lazima mwanaye aoelewe na Masoud ambaye ni shemeji yake kwa Naima, kama ni kuvunjika kwa undugu, iwe hivyo.
“Nilimtegemea kwa ushauri na malezi bora lakini kitendo cha binti yake kuchukua mume wa dada yake, naye kuunga mkono ni aibu,” alisema Wastara.
Wakati akiendelea kusimulia huku akitoa machozi, alimwambia mwandishi wetu anajisikia kizunguzungu kisha akalegea na kupoteza fahamu hali iliyomlazimu paparazi wetu kuomba msaada kwa jamaa zake waliokuwa nje ya gari.

Baada ya kama dakikia 15, Wastara alizinduka na muda mfupi baadaye alisema safari hii hatakubali kuona dada yake akiporwa mume huku ndugu zao wakichekelea na kwamba kama ‘mbwai mbwai tu’.
CHANZO:GPL

Popular posts from this blog

YEBOYEBO,MTINDO WA NYWELE UNAOPENDWA HADI SASA

MICHORO MBALIMBALI YA HINA

JINSI YA KUPAKA RANGI NDANI YA NYUMBA YAKO

Swala la kuchagua rangi inayofaa ndani ya nyumba huwachanganya wengi.Wengi hushindwa kuamua ni rangi gani wapake. Na endapo mtu atataka kuchanganya rangi za aina mbili au zaidi ni rangi gani atumie? Habari hii inaweza kuwasaidia kidogo kwani nitawawekea baadhi ya picha jinsi rangi zinavyoweza kupangiliwa na kupendeza.Kikubwa vilevile zingatia samani ulizonazo au unazohitaji kuweka katika nyumba yake ili usilete mchanganyiko wa rangi utakaoumiza kichwa.