Saturday 25 June 2016

AINA 10 ZA NDOA


1. NDOA YA MKEKA
Inatokana na kufumaniwa na Binti wa watu.
Ndoa hii huwa Haina mahari. Hii huvunjika mwaka mmoja tu,baada ya wanandoa kugundua hawakuwa wakipendana!
2. NDOA YA MIHEMKO
Hufungwa na vijana wenye umri wa miaka kati mume18 mke 16.Huvunjika baada ya miaka 3 au 4 ya ndoa.
 

4. NDOA YA MAONYESHO
Wenye ndoa Hii hupenda kujionyesha barabarani.Ila ndani hazina utii.Hupigana kila wanaporudi kutoka kwenye mizunguko. Cha kushangaza huwa hazivunjiki lakini ndiyo ndoa zinazoongoza kwa kuchepuka!

MAHUSIANO - MKE WA MTU Eps 01

LUV THE SHOES

Wednesday 22 June 2016

CHAGUO LANGU LA PICHA LEO

UREMBO WA HENNA!

Henna ni urembo mzuri kwa wanawake.Wachoraji wanatumia ubunifu mkubwa katika kuweka nakshi za kuvutia.
Michoro ya henna huchorwa sana miguuni na mikononi,ingawa wengine huchora katika sehemu nyingine mbalimbali za mwili.
Vilevile henna hutumika katika kubadilisha rangi ya nywele.Nitakuja kuandika makala ya henna katika nywele na faida zake!

UREMBO WA HENNA!

Henna ni urembo mzuri kwa wanawake.Wachoraji wanatumia ubunifu mkubwa katika kuweka nakshi za kuvutia.
Michoro ya henna huchorwa sana miguuni na mikononi,ingawa wengine huchora katika sehemu nyingine mbalimbali za mwili.
Vilevile henna hutumika katika kubadilisha rangi ya nywele.Nitakuja kuandika makala ya henna katika nywele na faida zake!

Monday 20 June 2016

NDUGU CHANZO CHA NDOA NYINGI KUVUNJIKA

Katika ndoa nyingi za Kiafrika; wanandoa huingia na msururu wa watu kwenye ndoa. Unakuta mke, mme ama wote wawili wana watu wanaowategemea, (extended family). Hawa watu wanaomtegemea mwenzi, kuna saa huwa ni chanzo cha migogoro katika ndoa. Kuna wanaotegemea kusomeshwa, wengine kulishwa, kuvikwa n.k. Mtegemewa akikwama kutimiliza mahitaji yao wanaanza maneno, visa, vitimbi n.k. Sana sana upande wa ndugu wa kiume ndiko huwa kuna shida zaidi. Ndugu wa kiume wakiona hawapati yote wanayotaka huwa wanainua vita dhidi ya mke (yaani wifi, shemeji na mkamwana wao); wakiamini kuwa ndie anaemzuia mumewe (kaka yao, kijana wao, ndugu yao) kuwasaidia. Ni vema wanandoa kufahamu mambo manne kuhusu hili: 1) Ndoa ni taasisi inayojitegemea na haitakiwi kuyumbishwa na matakwa ya wengine hata kama ni wazazi, mawifi, mashemeji n.k 2) Hata kama ukiwa/mkiwa na huruma kiasi gani hamuwezi kumsaidia kila anaekuja kutaka msaada na hata mkisema msaidie kila mtu hamuwezi kuwaridhisha wote. Maneno na lawama vitakuwepo tu. Kwa hiyo, kama wanandoa lazima mkae chini kwa pamoja mkubaliane ni watu gani wana ulazima wa kuwasaidia kutoka pande zote mbili(kikeni na kiumeni), kisha mnawasaidia kwa kadiri ya uwezo mlionao. Wengine acheni tu wawalaumu kwa maana lawama haziui! 3) Msijichoshe kuwasaidia ndugu kupita uwezo wenu, kumbukeni na ninyi ni familia mnahitaji pia maendeleo katika ndoa, mkiruhusu watu "wachotage tu", mtakwama halafu hao hao waliokuwa wanachota watageuka kuwasema 4) Katika wale mliokubaliana kuwasaidia tumieni mfumo wa kuwawezesha wajitegemee badala ya kuwapa kila siku. Wanaowezekana kusoma wasomesheni hata kozi tu ili wajitegemee, waliokataa shule watafutieni hata mitaji. Badala ya kutuma fedha kila mwezi kwa wazazi kule kijijini fanyeni ubunifu muwaanzishie japo miradi midogo midogo kama kufuga kuku, ngo'ombe, n.k. MWISHO: Katika wale mnaowasaidia msilee uzembe, kama mtu mnamsomesha lakini anakula ada ama kufanya uhuni, msimchekee! Kama mnampa mitaji lakini anashinda akiipoteza; msimvumilie. Kuna baadhi ya extendend family members ambao ili NDOA IWE NA USALAMA, ni lazima kufanya maamuzi magumu dhidi yao. Vinginevyo mnaweza kuvunja ndoa kwa kukumbatia ndugu wenye miiba miilini mwao(wasiobebeka).
CHANZO:Ni wakati wako wa kung'aa on facebook

Thursday 16 June 2016

I LOVE THIS HANDBAG DESIGN

SLIP-INS

THE GARDEN:NIMEPENDA MPANGILIO WA MAUA HAYA

KALI YA SIKU

NUKUU YA LEO:TUSILIPE WEMA KWA UBAYA

Tuepuka kulipa ubaya kwa aliyekufanyia mema.Utakuwa na furaha ya muda mfupi sana (kama utakuwa nayo).
Hii ndiyo KARMA.Utapata mema kama ukitenda mema na yatakupata mabaya zaidi ya uliyotenda ukitenda mabaya.
Tumeona wengi wameharibu kabisa mwelekeo wa maisha yao eidha kwa tamaa ya kupata zaidi au kwa ujinga tu.
Wa kujenga au kuharibu maisha yako ni wewe mwenyewe kutokana na matendo yako.Tuepuke kuumiza wengine kwa  kudhani tunajitengenezea au ndiyo tunakaribisha PEPO katika maisha yetu.Kumbe  ndiyo tunakaribisha ghadhabu ya Mungu.Hapa ndiyo mwanzo wa majanga kudhallilika na kufedheheka. Kwani ulichokifanya ni sawa na kukata tawi la mti ulilokalia  mwenyewe.Ni wewe ndiye utaanguka na si uliyemtendea mabaya.
Tuangalie matendo yetu kwa wengine!

SIKU NJEMA

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...