Friday 5 September 2014

VIUNGO 10 AMBAVYO NI LAZIMA KUWA NAVYO JIKONI KWANGU,JE WEWE VYAKO NI VIPI?



1.     PASTA
 Hiki ni chakula cha haraka.Unaweza kutayarisha pasta kwa kuongeza tu protini ulizonazo katika jokofu lako mfano kuku,nyama ya kusaga, kamba(prawns) n.k.Ili kuzifanya pasta zako ziwe tamu  pasha  ½ kikombe cha  mafuta ya zeituni(olive oil) kikaangoni,weka spinachi,nyanya au uyoga.Pika kwa dakika 3 au mpaka mboga zilainike. Ongeza chumvi na pilipili(kama unatumia pilipili).Changanya pasta zako ambazo zimepikwa tayari katika mchanganyiko huu wa mboga.

2.  CHICKEN BROTH OR BOUILLON
 Unaweza kutengeneza mchuzi au supu kwa kutumia chicken broth pamoja na viungo vingine ulivyonavyo jikoni kwako na kupata mlo mzuri kabisa. Mfano unaweza kuongeza mbogamboga au nyama nk.Unaweza kutumia hii katika kuongeza ladha kwenye kuku wa kuoka,kupikia wali na hata mbogamboga badala ya kutumia maji.



3.    MBOGA ZILIZOGANDISHWA/ZILIZOHIFADHIWA KATIKA KOPO
Unaweza kuzipasha kwa kuchanganya na chicken broth ukapata mchuzi au supu.Unaweza kuongeza ladha kwa kutupia vipande vya kuku na viungo vingine utakavyo kuweka ladha.
4.    KUKU
 Unaweza kupika kuku katika njia nyingi tofauti.Unaweza kuchanganya na mbogamboga, kumchoma/kuoka, kukaanga n.k.Mimi binafsi kuku na samaki zinakamilisha kabisa mlo wangu na huwa havikosekani jikoni kwangu.Kuku nzuri kuwa nayo ni ambayo ambayo imetolewa mifupa.
5.    VIAZI
Viazi kama ilivyo kwa kuku,huweza kutumika kutayarisha idadi kubwa ya chakula.Viazi huweza kutumika katika supu au mchuzi.Vilevile vinaweza kuokwa, kuchemshwa, kukaangwa katika aina nyingi tofauti.
6.    MAYAI
Hiki ni kiungo kikubwa na muhimu sana jikoni.Mayai hayatumiki kwa kifungua kinywa tu, huweza vilevile kutumika kutengeneza vyakula kamili.

7.    NYAMA YA KUSAGA
Hiki ni kiungo muhimu kwani unaweza kutengeneza vyakula tofauti kwa kutumia nyama ya kusaga mfano mkate wa nyama,meat balls, tacos, hamburgers n.k.Unaweza kuongeza ladha kwa kuongeza kitunguu thoum, pilipili manga/pilipili ya unga,chumvi n.k

8.    MCHELE
 Mchele unaweza kutumika kutengeneza mlo kamili  mfano  risotto, sushi, supu ya kuku na mchele, jambalaya au pilau. Aina tofauti za mchele zijulikanazo ni arborio, jasmine, basmati n.k

9.    NYANYA YA KOPO/BOKSI
:Nyanya ni kiungo muhimu katika mchuzi au supu. Unaweza kuchanganya nyanya na viungo tofauti na kutengeneza sosi yako mwenyewe kwaajili ya pizza au pasta.

10. BACON
Unaweza kutupia bacon katika pasta, viazi au supu na kuongeza ladha katika mlo wako.



No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...