Saturday, 31 August 2013

20 kusomea gesi na mafuta China, Brazil


Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu wanafunzi waliochaguliwa kwenda nchini Brazil na China kusomea shahada ya uzamili fani ya mafuta na gesi. Picha na Fidelis Felix 

Dar es Salaam. Watanzania 20 wamepata ufadhili kwenda China na Brazil, kusoma shahada ya uzamili katika fani ya gesi na mafuta, huku Serikali ikieleza kuwa mpaka sasa kuna pengo la wataalamu zaidi ya 200 kwenye sekta hiyo.
Kuchaguliwa kwa Watanzania hao ni utekelezaji ahadi iliyotolewa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, wakati akiwasilisha bajeti ya wizara hiyo mwaka 2013/14.

Profesa Muhongo alisema Serikali itawatafutia ufadhili Watanzania kusomea fani hizo, hasa baada ya kugundulika kwa kiwango kikubwa cha gesi na mafuta nchini.
Wizara hiyo ilitangaza mpango huo kupitia vyombo mbalimbali vya habari, zaidi ya vijana 100 waliomaliza shahada vyuo mbalimbali nchini walituma maombi, ambayo yalitumwa katika nchi hizo na kuchaguliwa 20.
Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Eliakim Maswi, alisema vijana 10 wanaokwenda China wataondoka Septemba 3, mwaka huu na kwamba kati yao, wawili wanatokea wizarani hapo.
Maswi alisema wengine 10 wanakwenda Brazil, lakini watalazimika kujifunza Lugha ya Kireno kwanza kwa muda wa miezi sita, kwani lugha hiyo ndiyo inayotumika nchini humo. Alisema sekta ya nishati inakabiliwa na changamoto mbalimbali.
, kama upatikanaji umeme, kuendeleza sekta ya gesi, kuendeleza vyanzo mbadala vya nishati na kuacha kutegemea maji,” alisema Maswi na kuongeza:
“Pia, tunahitaji wataalamu wa gesi na mafuta zaidi ya 200, hivyo licha ya kuwapeleka hawa, pengo ni kubwa na tutaendelea kuwasomesha wengi zaidi, wakiwamo kutoka wizarani.
CHANZO: MWANANCHI

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...