Saturday 24 August 2013

RAIS JAKAYA AKIWAAPISHA MAKATIBU WAKUU NA MANAIBU WAPYA WA WIZARA MBALIMBALI LEO IKULU LEO JIJINI DSM

Rais Jakaya Kikwete (kushoto) akimuapisha Naibu Katibu Mkuu Mpya wa Wizara ya Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo, Prof.Elisante Ole Gabriel Laizer ( kulia) leo katika hafla Ikulu Dar es Salaam ,PICHA NA MWANAKOMBO JUMAA WA MAELEZOdo9 
Rais Jakaya Kikwete (kushoto) akimuapisha Katibu Mkuu Mpya wa Wizara ya Habari ,Vijana , Utamaduni na Michezo Sihaba Nkinga (kulia) leo katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam. 5-jk akimuapisha mama shel-(kulia) 
Rais Jakaya Kikwete (kushoto) akimpongeza na kumkabidhi zana za kufanyia kazi  Naibu Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Rose Shellukindo (kulia) 

Picha ya pamoja ya Waziri wa Hbari , Vijana , Utamaduni na Michezo Dkt, Fenella Mukangara (wapili kulia mstari wa mbele) Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amos Makalla(kulia mstari wa mbele), Katibu Mkuu mpya wa Wizara hiyo, Sihaba Nkinga(mwenye mauawa) ,Naibu Katibu Mkuu mpya Prof. Elisante Ole Gabriel Laizer (wa kwanza kashoto mwenye miwani) pamoja na baadhi ya  wakurugenzi wasaidizi katika  wizara hiyo na baadhi ya  watendaji, wakuu wa wizara, 
 7- CDF Mwamunyange  na JK (kushoto) wakisalimiana 
Rais Jakaya Kikwete (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Majeshi ya JWTZ, Jenerali Davis Mwamunyange (kulia) wakati wa sherehe za kuwaapisha Makatibu wakuu wapya pamoja na Manaibu Katibu wakuu waWizara mbalimbali leo katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam. 8-jk akimuapisha mama mwamunyange (kulia) 
Rais Jakaya Kikwete (kulia) akimuapisha Naibu Katibu Mkuu Mpya wa Wizara ya Uchukuzi, Monica Mwamunyange.(kulia). 9-picha ya pamoja 
Picha ya pamoja  akiwepo na Rais Jakaya Kikwete ( wa sita kutoka kulia mstari wa mbele) akifuatiwa na Makamu wa RaisDkt. Muhamaed Gharib Bilal.pamoja na Makatibu Wakuu wapya na Manaibu wake,

 Rais Jakaya Kikwete na Katibu Mkuu Kiongozi Mhe Ombeni Sefue wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa ofisi ya Sekretariate ya Baraza la Mawaziri ambako watumishi wake wawili wameteuliwa kuwa manaibu Makatibu wakuu, ambao ni Injinia Angelina Madete (kulia kwa Rais) na Mhe. Consolata Mgimba (kushoto kwa Rais) mara baada ya kuapishwa Makatibu wakuu na Manaibu Katibu wakuu Ikulu jijini Dar es salaam leo.
 Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilal na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika picha ya pamoja na Makatibu wakuu na manaibu Katibu wakuu wapya mara baada ya kuapishwa Makatibu wakuu na Manaibu Katibu wakuu Ikulu jijini Dar es salaam leo.
 Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilal na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika picha ya pamoja na Makatibu wakuu wapya mara baada ya kuapishwa Makatibu wakuu hao na Manaibu Katibu wakuu Ikulu jijini Dar es salaam leo.

Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilal na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika picha ya pamoja na Manaibu Katibu wakuu mara baada ya kuapishwa Makatibu wakuu na Manaibu Katibu wakuu hao Ikulu jijini Dar es salaam leo.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo,Ijumaa tarehe 23 Agosti, 2013, katika viwanja vya Ikulu, amewaapisha Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu.

Ifuatayo ni Orodha ya Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu walioapishwa leo.

1.    MAKATIBU WAKUU

Ndugu Sophia Elias Kaduma
Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika

Ndugu Jumanne Abdallah Sagini
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)

Ndugu Uledi Abbas Mussa
Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda na Biashara

Dr.  Patrick James Makungu
Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia


Ndugu Alphayo Japani Kidata
Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Ndugu Charles Amos Pallangyo
Katibu Mkuu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii

Ndugu Sihaba Said Nkinga

Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo

Ndugu Anna Tayari Maembe
Katibu Mkuu, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto

2.    NAIBU MAKATIBU WAKUU
Ndugu Dorothy Stanley Mwanyika
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha (Fedha za Nje na Madeni)

Ndugu Consolata Philipo Mgimba
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi

Eng.  Angelina Elias Augustine Madete

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais

Dr. Deodatus Michael Mtasiwa
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, (TAMISEMI) - AFYA

Ndugu Monica Lyander Mwamunyange

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Uchukuzi

Ndugu Regina Lucian Kikuli
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu

Ndugu Kagyabukama Edwin Kiliba
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, (TAMISEMI)

Ndugu Zuberi Mhina Samataba
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, (TAMISEMI) - ELIMU

Dr. Yamungu Kayandabila
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika

Prof. Adolf Faustine Mkenda
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha (SERA)

Ndugu Mwitango Rose Shelukindo
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

Dr. Selassie David Mayunga
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Prof. Elisante Ole Gabriel Laizer
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo

Ndugu Amantius Casmiri Msole
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki


Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu

Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...