Friday 30 August 2013

WALIOFUKUZWA TAZARA WAREJESHWA



Mkurugenzi Mkuu wa Tazara,Ronald Phiri

Mkutano wa bodi ya Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia (Tazara) ,imetengua maamuzi ya kuwafukuza wafanyakazi 1,067 na kuagiza warudishwe kazini, agizo hilo linamtaka kila mfanyakazi kuendelea na kazi huku mishahara ikishughulikiwa.

Mkurugenzi Mkuu wa Tazara, Ronald Phiri, alisema jana pasipo kutaja sababu kuwa yeye aliagizwa na bodi kutangaza kurejea kwa wafanyakazi hao kama alivyotangaza awali kufukuzwa kwao.

“Siku mbili zilizopita nilitangaza wafanyakazi 1,067 niliwafukuza kazi, lakini leo natangaza warudi kazini na kuendelea na kazi,” alisema Phiri na kuongeza kuwa hatua hizo zimechukuliwa kwa kuwa hakuna mfanyakazi aliyepewa barua ya kufukuzwa na kuhesabika kuwa bado ni wafanyakazai wa Tazara.

Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Reli Tanzania (Trawu), Mussa Kalala, alisema hakuna mfanyakazi atakayerudi kazini hadi mishahara itakapolipwa.

Alisema kuwa wataweza kurudi ikiwa wajumbe wa bodi watafika Tazara na kuzungumza na wafanyakazi.
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...