Iringa ni mojawapo ya miji ya kihistoria nchini Iringa ilianzishwa mwaka 1892 kama kambi la jeshi la kikoloni wakati wa vita ya Wajerumani dhidi ya Wahehe. Wahehe waliongozwa na kiongozi wao,Chifu Mkwawa ambaye makao yake makuu yalikuwa Kalenga. Asili ya jina la Iringa ni neno la Kihehe "liliga" lenye maana ya boma. Mji umejengwa juu ya mlima ukitazama mto Ruaha bondeni.
Mji wa leo upo mahali pa "Neu Iringa" au Iringa mpya ya Wajerumani waliotumia jina hili baada ya kuharibu boma la mtemi Mkwawa huko Kalenga waliloita "Iringa" tar. 31 Oktoba 1894.
Mkoa wa Iringa una vivutio kadhaa vya utalii kama Isimila, jiwe la Gangilonga, makumbusho ya mkwawa huko Kalenga, mbuga za Ruaha n.k.Tuanze safari ya kuutembelea mji wa Iringa na vivutio vyake katika picha!
Picha juu zinaonyesha mwonekano tofauti wa mji wa Iringa
Stendi kuu ya mabasi-Iringa
Mapango ya Kitwiru ambapo Mkwawa na majeshi yake walijificha na kupanga mashambulizi dhidi ya Wajerumani.Mapango haya yapo umbali wa kilomita 5 toka Iringa mjini.
Used to teach physics at Mkwawa High School in the 1960s - Rod stanley
ReplyDelete