Wednesday 18 September 2013

MWINJILISTI MWANAMKE AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUWATUNZA WAHAMIAJI HARAMU


7
 Mwiinjilisti  mwanamke  kutoka nchini Nigeria  ambaye ana kibali cha kazi ya uinjilisti  katika  huduma ya Life Changer  Chapel  iliyoko Sinza  jijini Dares Salaam , Blessing  Dangana, anayedaiwa kuwatunza raia wa Nigeria watano ambao wanatoa huduma hiyo bila kibali maalum akitoka nje ya Mahakama ya  Hakimu Mkazi ya Kisutu mara baada ya kufikishwa mahakamani hapo jana.
1
 Baadhi ya raia wa Nigeria wanaodaiwa kutunzwa  Mwinjilisti mwanamke  mwenye kibali cha kazi hiyo Blessing  Dangana   katika  huduma ya Life Changer  Chapel  iliyoko Sinza  jijini Dares Salaam , wakitoka  nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu mara baada ya kufikishwa mahakamani hapo huku wengine wa kijificha sura zao.

4
5
Gari la Idara ya Uhamiaji likiwa limebeba baadhi ya raia wa Nigeria wanaodaiwa kutunzwa  Mwinjilisti  mwanamke mwenye  mwenye kibali cha kazi hiyo Blessing  Dangana   katika  huduma ya Life Changer  Chapel  iliyoko Sinza  jijini Dares Salaam hao mara baada ya kutoka mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu jijini Dares Salaam.
3
Baadhi ya vijana wanaodai kuwa wanatoka mkoa wa Kigoma  wakiwa wajaza fomu ambao taarifa zao zinaendelea kuchunguzwa  kama  kweli ni Watanzania wakiwa katika Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam.(Picha zote na Magreth Kinabo- Maelezo).

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...