Kamishna Suleiman Kova |
Kufuatia kukithiri kwa matukio ya uhalifu wa kupora fedha kwenye mabenki jijini Dar es Salaam, kuanzia leo benki zitakuwa zinalindwa na Jeshi la Polisi.
Aidha, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia mtu mmoja mwenye asili ya kiasia, kwa tuhuma za kuhusika katika matukio hayo uliofanyika hivi karibuni.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Kamishna Suleiman Kova, alisema uamuzi wa kulinda benki umefikiwa kufuatia mkutano kati yake na Makamanda wa Polisi wa Mikoa wa Kanda hiyo.
Kamannda Kova alisema wamekubaliana mambo kadhaa ili kuhakikisha uhalifu huo unaofanywa na magenge ya kihalifu unadhibitiwa na kwamba makamanda hao wametakiwa kuhakikisha kuwa wanashiriki kikamilifu katika utekelezaji wake.
Wakati huohuo Kamanda Kova alisema Jeshi hilo limefanikiwa kumkamata Azim Chokera (47) kwa tuhuma za kuhusika katika matukio yote mawili.
La kwanza ni la juzi na lile la mwishoni mwa wiki ambayo mabilioni ya fedha yaliibiwa na watu waliovalia sare za Jeshi la Polisi na Chokera akionekana akiingiza ndani ya benki hizo na kutoa maelekezo kwa wenzake kwa njia ya simu.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment