Saturday 14 September 2013

SAFARI YANGU KATIKA HIFADHI ZA TAIFA SAADANI KUPITIA PANGANI,TANGA










Mto Pangani,Tanga

Pangani,Tanga.Kilichonivutia ilikuwa ni uoto wa asili unaoonekana pembeni ya mto nyuma ya nyumba zinazoonekana).Ni muhimu kuhifadhi uoto huu kwani misitu ni muhimu katika upatikanaji wa mvua.


Nilivuka kwa kivuko hiki kutokea Tanga mpaka Mkwaja,halafu kuelekea Saadani. Saadani ni mbuga pekee ambapo mtu anaweza kuona wanyamapori wakivinjari pwani.


Twiga katika hifadhi za Saadani.Nilipiga picha hii baada ya kuzunguka kwa muda mrefu mbugani bila ya kuona mnyamwa yeyote zaidi ya ngiri ambao walikuwa wanazunguka katika ofisi za hifadhi.Saadani ipo katka ya wilaya ya Pangani (Tanga) na Bagamoyo, Pwani.

Wadau, ni vizuri kufanya utalii wa ndani kwani ni wengi ambao hawajawahi kutembelea vivutio vya utalii ambavyo nchi yetu imejaliwa.
Imeandikwa na Anna Nindi



No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...