Thursday 19 September 2013

TANGAZO LA UFADHILI KWA WASANII CHIPUKIZI WA FILAMU NA MUZIKI


TANGAZO LA UFADHILI KWA WASANII CHIPUKIZI WA FILAMU NA MUZIKI.

1. Wewe ni msanii chipukizi wa filamu au maigizo ?
2. Wewe ni mwandishi chipukizi wa filamu ?
3. Wewe ni mtayarishaji chipukizi wa filamu ?
4. Wewe ni muimbaji / mwanamuziki chipukizi Unataka kukamilisha ndoto zako lakini haujui pa kuanzia ?
Kama jibu ni ndio basi hii ni habari njema sana kwako.
Taasisi ya RafikiElimu Foundation inapenda kuwatangazia wananchi wote kuwa sasa, tumeanza kutoa ufadhili na udhamini kwa wasanii chipukizi wa filamu, waandishi chipukizi wa filamu, watayarishaji (Producers) chipukizi wa filamu pamoja na waimbaji(wanamuziki ) chipukizi wenye sifa zifuatazo :

1. Awe na kipaji cha kuigiza AU
2. Awe na kipaji cha uandishi wa filamu AU
3. Awe na nia thabiti ya kuwa mtayarishaji wa filamu AU
4. Awe na kipaji cha uimbaji.
5. Awe raia wa Tanzania na mkaazi wa jijini Dar Es salaam.
6. Awe na umri wa kuanzia miaka 14 hadi 55.

UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI

Tuma maombi yako kupitia barua pepe yetu ambayo ni : rafikielimutanzania@gmail.com . Maombi yaelekezwe kwa Mkurugenzi Mtendaji,RafikiElimu Foundation, S.L.P 35967, Dar Es salaam.
CHAZO: Michuzi

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...