Wednesday 14 May 2014

JB,IRENE UWOYA,MZEE MAJUTO NA RAY KWENDA UTURUKI KIKAZI

Wasanii wa filamu Jacob Stephan aka JB ,King Mjuto, Vicent Kigosi aka Ray na mwanadada Irene Uwoya wanatarajia kuondoka usiku wa kuamkia Jumatano hii kwenda Uturuki kujifunza utamaduni za nchi hiyo pamoja na kukutana na waigizaji wakubwa wa nchi hiyo.

Uongozi wa Uturuki pamoja na wasanii wa filamu
Uongozi wa Princess Casino pamoja na wasanii wa filamu
Wasanii hao ambao amepata udhamini Princess International Casino wamesema safari hiyo ya wiki moja wataitumia kwenda kujifunza mambo mbalimbali yatayowasidia kukuza sanaa yao. Akizungumza na waandishi wa habari akiwa Princess Casino ndani ya IT Plaza Jijini Dar es salaa, mmoja kati ya wasanii hao,Jacob Stephan amesema kuwa wameahidiwa na Princess International Casino kwenda kukutana na watu muhimu kwenye tasinia yao.
“Princess Casino wametuahidi kule tutakutana na watu muhimu sana kwenye shughuli ambayo tunafanya,kwangu mimi naiita hii ni fursa kwasababu ni vitu ambavyo tulikuwa tunaomba,” alisema.  


 Pia kwa upande wake mchekeshaji mkongwe King Majuto amedai kuwa katika safari hiyo atajifunza na kuangalia tamaduni za watu wa Uturuki.
“Mimi nimefurahi sana kwenda Uturuki,huu ni mwanzo mutasikia Majuto kahamia Uturuki, safari yangu ni kujua utamaduni wao,mimi nimefarijika sana kwenda kubadilisha mawazo kwa mapuMziko. Hii ni heshima kubwa sana kwangu haswa,kwasababu niliganda hapa mpaka nafa, leo nimepata faraja ygingine tena isije ikaniua,” alisema.

Ray na Mzee Majuto
Ray na Mzee Majuto

Show za watu za Tamaduni za Ururuki zikendelea - Copy
Show za watu za Tamaduni za Uturuki zikendelea
JB na Irene Uwoya
JB na Irene Uwoya
Mzee Majuto na Zamaradi
Mzee Majuto na Zamaradi
CHANZO: Bongo5

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...