David Moyes (50) amesaini mkataba wa  miaka 6 kuinoa timu ya Manchester United. David anarithi mikoba wa kocha Alex Ferguson.Moyes anatokea timu ya Everton.
“Ni heshima kubwa kuwa meneja wa timu ya  Manchester United,”alisema Moyes katika taarifa yake.
“Nina furaha kuwa Sir Alex  ameniona ninafaa na hivyo kunipendekeza mimi kwa kazi hii. Nina heshima kubwa kwa kila kitu ambacho  Sir Alex amekifanya na kwa timu.”
Jumatano iliyopita,Ferguson   alitangaza kuwa anastaafu kazi ya umeneja nafasi ambayo amekuwa nayo kwa karibu miaka 27 Old Trafford.
CHANZO: Northjersey sports

No comments:
Post a Comment