Aziza Masoud, Mwananchi
Imeelezwa kuwa Benki ya Damu ya Taifa, imeshindwa kufikia malengo ya ukusanyanji wa damu na badala yake ime kusanya chupa 120,000 kati ya 400,000 zinazohitajika kwa mwaka.
Akizungumza mwishoni mwa wiki katika maadhimisho ya siku ya kuchangia damu yaliyofanyika wilayani Kibaha, Mkurugenzi wa Afya wa Chama cha Msalaba Mwekundu, Bertha Mlai, alisema kwa mujibu wa taarifa za Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Tanzania ina uhitaji mkubwa wa damu.
“Damu inayokusanywa na Benki ya Damu nchini kwa mwaka ni sawa na asilimia 26 hii inaonyesha upungufu mkubwa wa upatikanaji wa damu,” alisema Mlai.
Alisema watu wengi wanapenda kuchangia damu wakati ndugu au rafiki anapokuwa akihitaji na kwamba hiyo inatokana na uhamasishaji mdogo.
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Halima Kihemba, alisema wananchi wanapaswa kuchangia damu kwa kuzingatia mahitaji makubwa ya damu.
No comments:
Post a Comment