Gereza la Robben
Rais Obama na mkewe Michelle wakitembea katika gereza la Robben karibu na mji wa Cape town.
Obama akisaini kitabu cha wageni
Huu ndiyo ulikuwa ujumbe aliouandika,ujumbe wake aliumalizia kwa kuandika "no shackles or cells can match the strength of the human spirit".
Obama alitumia muda katika chumba kidogo(selo) alichokuwa akilala Nelson Mandela
Hili ni eneo ambalo wafungwa akiwemo Mandela,walifanyishwa kazi
Obama alitembezwa na mwanasiasa wa zamani aitwae Ahmed Kathrada mwenye umri wa miaka 83 ambae alifungwa pamoja na Mandela.Kathrada alimwambia Obama kuwa wafungwa walifanyishwa kazi kila siku.Mandela alikaa katika gereza hilo kwa kipindi cha miaka 18 katika selo ndogo.Ni katika gereza hili ambapo Mandela alipata matatizo ya mapafu yanayomsumbua hadi sasa.
BBC & THE EXPRESSE
No comments:
Post a Comment