Mimi nina utaratibu wa kuweka kumbukumbu za manunuzi
yote ninayofanya.Vilevile nchini Sweden ambapo ninaishi unaponunua chochote
hupewa risiti hata kama ni ndizi moja.Huombi risiti bali unapewa kama haki yako
mnunuzi.Kaka yangu alisema angeifuata siku ya pili kwani kwa siku ile muda wa
kufunga duka ulikuwa umepita tayari.
Siku ya pili alikwenda dukani na wakawa wanampa
majibu yasiyoeleweka kuashiria kuwa hawatoi risiti.Akanipigia simu kunipa
taarifa na mimi nikamwambia nitakutana nae dukani baada ya muda mfupi.Baada ya
muda nikawa nimefika dukani.
Bahati nzuri walinikumbuka maana nilikwenda na kaka
yangu siku iliyopita.Dukani pale walikuwepo wauzaji wawili.Mimi sikuwa na swala
lingine zaidi ya kuwaomba risiti yangu.
Wakaanza kutaka kunizungusha na
mimi.Niliwaambia kitu kimoja tu kuwa ``nipeni risiti yangu niondoke kwa
amani,nikiondoka hapa bila risiti basi mjue duka hili litafungwa kwani mnaiibia
serikali.``
Ukweli waliogopa sana na wakaanza kupigiana simu wahusika.
Naona wakaambiwa wanipe risiti.Nikapewa risiti yangu!
Unajua nini,VAT ya manunuzi niliyofanya ilikuwa
147,000/-!
Hizo ni pesa ambazo wasingepeleka serikalini bali
wangeingiza kwenye mifuko yao.Nikawaambia mimi ninajua haki ya mnunuzi ni ipi
na ninajua kwanini hawataki kutoa risiti kwa watu kwasababu wanaiibia
serikali.Ila pale nilikuwa nazungumza kwa niaba yangu mwenyewe na
sikumzungumzia mtu kwa kuwa mimi ndiye nilitoa pesa za manunuzi yale
yaliyofanywa.Kitu cha ajabu ,baadhi ya wateja waliokuwepo dukani pale
walionekana kunishangaa kabisa masikini.
Wengine wakawa wanasema wao hawajui nini maana ya
risiti.Nilichojifunza pale ni kuwa wananchi wanahitaji kuelimishwa.Mamlaka ya
mapato wakitoa elimu nzuri kwa wananchi ujanjaujanja kama huu utakwisha.
Wafanyabiashara wengi huogopa watu wanaoelewa sheria
na haki zao.Wananchi wanatakiwa kujua kuwa risiti wanapofanya manunuzi ni HAKI
yao.
Watu tunailaumu serikali kwa kukosa madawati katika
mashule,vitanda vya kutosha mahospitalini n.k.Serikali inaweza kufanya hayo
yote kama kodi italipwa kihalali na kwenda mahali panapohusika ili kufanya
shughuli za maendeleo.Nchi zote zilizoendelea duniani,kodi inakusanywa na
inafanya shughuli za maendeleo ikiwemo kuboresha afya,elimu,ustawi wa jamii nk.
Hivyo mwananchi dai risiti kila unapofanya manunuzi
kwa maendeleo ya nchi yako.
Imeandikwa na
Anna Nindi
No comments:
Post a Comment