Ujumbe mzuri kutoka kwa wakina baba maana bila wao ukatili huu hautakwisha
Ukeketaji unafanyika hasa barani Afrika, lakini unafanyika pia katika nchi fulani za Asia na Amerika ya kusini.
Sababu hizo ni pamoja na kutunza ubikira kabla ya ndoa, kupunguza hamu ya kutaka kujamiiana na kuondoa nafasi ya kuwa na uhusiano wa mapenzi nje ya ndoa halali au mwenza kujitunza na kuondoa uwezekano wa kupata maambukizi ya ugonjwa yanayosababisha na uchafu unaojulikana kama lawalawa, kuwaongezea wanawake starehe ya tendo la ngono wakati wa kujamiiana kutokana na kutokuwapo kinembe na maji maji ukeni.Kwangu mimi naona huu ni mtazamo hasi.Ina maana asietakiwa kutembea nje yya ndoa ni mwanamke tu?
Je,wanaume hufanywa nini ili wao wasitembee nje ya ndoa?
Vita ya kutokomeza ukeketaji si ya mtu mmoja au taasisi moja.Vita ya kutokomeza ukeketaji inatakiwa iongozwe na jamii yote vinginevyo ukeketaji hautakwisha.Wanawake tusimame na kuonyesha kupinga kwetu kitendo hiki kwa vitendo ikiwemo kukataa kukeketa watoto wetu.Wakina baba mtasaidia sana katika harakati hizi kama nyinyi hamtakubali kuoa wanawake waliokeketwa.Elimu mbalimbali itolewe kwa wananchi hasa vijijini kuhusu madhara ya ukeketaji.Tukiungana katika hili nina uhakika kuwa vita hii tutaishinda.
Tutokomeze ukeketaji ili kulinda afya na utu wa mwanamke na mtoto wa kike.
Imeandikwa na Anna Nindi
No comments:
Post a Comment