Wednesday, 19 June 2013

VURUGU ZA ARUSHA JUMATATU 18/6/2013 TAARIFA YA JESHI LA POLISI



Taarifa za sasa kutoka kwenye jeshi la Polisi Arusha kuhusu vurugu za jana June 18 zilizofanya mpaka mabomu ya machozi kupigwa kwenye mitaa mbalimbali ya Arusha, ni watu 67 wanashikiliwa na polisi kutokana na vurugu za jana katika mkutano wa Chadema.Polisi wanasema leo  watu hawa wakiwemo wabunge wanne ambao ni Tundu Lissu, Mustapha Akunai, Mama Nkya na Said Hafizi watafikishwa Mahakamani wakati wowote.

Polisi wamemtaka Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe popote alipo ajisalimishe ili kulisaidia Jeshi kwa sababu alitamka kwamba ana ushahidi wa kutosha kwamba bomu la juzi lililoua watu kwenye mkutano wa Chadema lilirushwa na Polisi.Wanasema kama hatopenda kulipa Jeshi la Polisi ushirikiano basi apeleke ushahidi huo kwenye ofisi yoyote ya Serikali anayoiamini au hata kwenye ofisi ya Rais, anaweza kumkabidhi mkuu wa Nchi pia.
Chanzo: Clouds

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...