Katibu wa Wabunge wa Tanzania Katika Bunge la Afrika Mashariki, Shy-Rose Bhanji akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu miswada mbalimbali iliyojadiliwa na bunge hilo kwa kipindi cha mwaka mmoja. Kushoto ni mbunge wa bunge hilo, Abdullah Mwinyi. Picha zote na Habari Mseto
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Abdullah Mwinyi akizungumza na waandishi wa habari leo. Kulia ni Katibu wa wabunge wa Tanzania katika bunge hilo, Shy-Rose Bhanji.
Na Mwandishi Wetu, Dar, Tanzania
KATIBU wa Wabunge wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki, Shy-Rose Bhanji, amejivunia harakati chanya alizoshiriki katika kipindi cha mwaka mmoja tangu kuanza kushiriki vikao vya bunge hilo Juni mwaka jana, huku akiielezea kuvutiwa na miswada miwili inayosubiri baraka za Marais wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Shy-Rose, alisema kuwa, yeye kama mbunge amejifunza mengi katika miezi 12 ya uwapo wake bungeni, huku akiitaja miswada hiyo kuwa ni sheria ya Udhibiti wa Uzito wa Magari Barabarani ‘Vehicle Load Contol Bill’ na Punguzo la Vituo vya Ukaguzi Mipakani ‘One Stop Border Posts Bill.’
Aliongeza kuwa, bunge hilo limeijadili kwa kina miswada hiyo, ambayo kwa sasa inasubiri maamuzi ya Marais wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, huku akitoa wito kwa wafanyabiashara kutumia fursa za Kijiografia za Afrika Mashariki ili kujiletea maendeleo yao na taifa kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment