Miss Tanzania mwaka 2006 na muigizaji wa filamu Wema Sepetu amefunguka kupitia jarida jipya la Mzuka kuwa katika uhusiano wake wote na Diamond hakuwahi kumsaliti.
Wema ambaye yupo kwenye cover la jarida hilo linalotolewa na Bongo5,amefunguka kwa kusema kuwa yeye na Diamond walikuwa wakipendana sana.
“Maisha yangu yote tangia nimeanza mapenzi na Naseeb naweza kusema kuwa sikuwahi kuwa unfaithful. I used to be very faithful to him na tulikuwa tunapendana sana. With Naseeb nilikuwa nimesharidhika na maisha ambayo niko nayo,” amefunguka Wema.
Wema amefunguka pia kuhusu jinsi Diamond alivyomcheat na Jokate kwa kusema, “nadhani pia inacost mwanaume akishajua kwamba anakutawala in one way or another so labda ni shetani au ni ibilisi alimuingilia baada ya kutaka kuanza kushoot video ya Mawazo ndo rumors zilianza, nikawa siamini kwanza.”
Katika jarida hilo ambalo linauzwa kwa shilingi 1,500 tu, Wema amesimulia mengi tangia alipokutana na Diamond, jinsi alivyoumizwa na kitendo chake cha kumrekodi na kusambaza sauti kwenye radio, mapenzi yake na Kanumba, utajiri wake, jinsi anavyowapenda mbwa wake na mambo mengine exclusive.
No comments:
Post a Comment