Tuesday 9 July 2013

AMA KWELI DAWA ZA KULEVYA NI HATARI-NI MANENO YA MSAFIRI DIOF.

Diof-Picha kutoka maktaba


By Vicky Kimaro, Mwananchi
Diouf ambaye alikiri kutumia madawa hayo toka mwaka 1996 alisema alikata shauri mwenyewe na kwenda kutibiwa kwenye hospitali ya Lutindi iliyopo Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga.
“Nilianza kubwia unga toka mwaka 1996, sikujua kama unga una madhara, awali nilikuwa navuta bangi lakini kuna jamaa mmoja sasa hivi ni marehemu ndio alinifundisha kubwia unga.”
“Kuna wakati alikuwa anachanganya unga na bangi. hata hivyo mimi na wenzangu hatukujua kama anachanganya na bangi, kuna siku akatupa bangi bila ya kuchanganya na unga tulivyovuta tukaona mbona ipo tofauti na haileti ulevi sana, tukamuliza hii vipi mbona mbaya akasema sijawachanganyia, tukamuuliza hujatuchanganyia na nini akasema unga, tukamwambia tuchanganyie basi, kweli alipochanganya tukavuta tukajiona kama tuko Ulaya vile, dunia yote ipo mikononi mwako.”

“Kuanzia hapo ndio nikafungua ukurasa mpya wa kutumia dawa za kulenya, nikafikia kipindi nikaacha kuchanganya na bangi, nikawa nabwia na kunusa, wakati ule kete moja ilikuwa ikiuzwa Sh 250 sasa hivi inauzwa Sh 2,000.”
“Uteja ni kitu ambacho kinaweza kukudhoofisha, mimi ulikuwa ukinidhoofisha kwani nilikuwa siwezi kupanda stejini kuimba kama sijabwia, nilikuwa mteja msafi, kipindi cha mwazo watu walikuwa hawajui kama mimi ni teja, ila wale wa karibu wakawa wananiambia mbona sauti inabadilika kama inakwaruza na kukauka.”
“Ilifika wakati mwili ulidhoofu, Diofu wa leo sio yule sasa hivi nina afya hata wewe si unacheki, nilikonda sana nilifikia hatua nikawa nikilala saa 10 usiku tunapomaliza kuimba siamki mpaka saa moja usiku, na nikiamka nakula kisha lazima nibwie ndio nitajisikie freshi.
ILIKUWAJE AKAACHA:
“Unajua mwanzoni mke wangu na ndugu zangu walikuwa wakinikamata kwa nguvu na kunipeleka hospitali, basi nikajikuta naacha na kurudia, sikuwahi kuacha moja kwa moja kama ilivyo sasa.”
“Nina watoto wawili, Najma a.k.a Vannesa na Taslim a.k.a Paris’ sasa roho iliniuma sana siku moja watoto wenzao walikuwa wanawaambia baba yenu nyie ni teja.
“Nilijisikia vibaya kuona watoto wangu watazidi kusakamwa kwa kuambiwa kuwa baba yao (mimi)ni teja.
“Hali hiyo ndio iliyonifanya niamue kukata shauri na kwenda Muhimbili nikaonana na Dokta Ayubu ambaye yeye akanipeleka Lutindi, hiyo ilikuwa ni mwaka jana na nilikaa hospitali kwa miezi mitatu lakini toka nimetoka huko nina miezi tisa na bado naendelea kupata ushauri Muhimbili, huwa naenda kila Jumatano na Ijumaa.”
WASANII KUPOTEZA MAISHA KWA AJILIYA UNGA
“Wasanii wengi wanatumia dawa za kulevya, wengi nimewaona wamedhoofika, namshukuru Mungu kwa kunitoa katika janga hilo.”
ALIJISIKIAJE ALIPOFIKA HOSPITALI KWA MARA YA KWANZA
“Sio siri unga unatoka mwilini kwa saa 72 yaani siku tatu, na ndio maana ukikosa kutumia siku moja tu lazima utaharisha sana na kutapika, utatetemeka kama mgonjwa wa malaria na unaweza kupoteza maisha usipopata, ndio maana ukishabobea wengine wanakuwa maskini, kwa sababu upo tayari kuuza chochote mradi upate hela ya kununua unga.”
“Mimi nilipofika Lutindi nilipatwa na hali hiyo sana, nikawa napiga kelele kama kichaa, yaani unaomba wakupe hata kidogo tu, lakini walichokuwa wanafanya ni kunichoma sindano ya usingizi maana bila sindano huwezi kupata usingizi.
Huko Lutindi sikuwa peke yangu, nilikuta watu kibao huko wengine walikuwa wameathirika mno hasa wale waliokuwa wakijidunga sindano, mimi namshukuru Mungu sikufikia kujidunga.”
ANASHAURI NINI WASANII WENZAKE:
“Wasanii ambao wanatumia unga wanitafute namba yangu ni 0777 926111 kama kweli kuna ambaye anataka kuacha kutumia unga kwa hiyari yake tena, nawahakikisha ataacha bila hata ya kuumia” anasema Diouf huku akionekana kujutia kujiingia kwenye vitendo hivyo vya ulevi.
ASHA BARAKA ANAMZUNGUMZIAJE DIOFU?
“Diouf bado ni mfanyakazi wa Asset, na moja ya mikakati ya Kampuni yetu si tu kuwatumia wasanii bali pia kuwajali afya zao, mara nyingi tumekuwa tukimsaidia katika matibabu yake mara kwa mara na sasa hivi vita yetu kubwa tunayopigana nayo ni kuhakikisha anaacha kunywa pombe.
“Ugomvi wetu sasa hivi kwa Diofu ni pombe tu, naamini akiacha Pombe hata matibabu yake atayafanya vizuri zaidi na ndio maana tumemsimamisha mpaka kwenye maonyesho yetu ili apate matibabu yake vizuri.”
Baraka anasema kuwa licha ya kumsimamisha kwenye maonyesho yao wamekuwa wakimpa stahiki zake zote ikiwemo posho na kumpongeza rapa huyo kuwa balozi mzuri wa vijana katika kupiga vita dawa za kulevya nchini.
“Aisha Madinda aliingia kwenye huo mkumbo, akatoka bendi yetu na kwenda bendi nyingine, tumemsaidia sasa hivi anaendelea vizuri, tupo kwenye mpango wa kumrudisha Twanga, na safari hii sio tu atanengua, pia atajifunza mambo mengine kama uimbaji na vitu vingine,”anasema.
Aisha Madinda ambaye ni mnenguaji wa bendi ya Extra Bongo, baada ya kutumia dawa za kuondoa sumu hivi sasa ni muhamasishaji kwa ‘mateja’ ambao bado wanatumia ‘unga’.
Madinda alikaririwa siku za hivi karibuni akisema bado anaendelea na matibabu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, pia amepewa kazi ya uhamasishaji katika Shirikia la Kudhibiti Madawa ya Kulevya na Ukimwi (PHRP) lililopo Kinondoni.

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...