Sunday 28 July 2013

HAUSIBOI ALIYEMLAWITI BINTI WA MIAKA MINNE AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA JELA HUKO MPANDA


Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi imemhukumu kijana, Baraka Juma (22) mkazi wa kijiji cha Nkungwi wilayani humo, kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kosa la kumlawiti mtoto wa kike mwenye umri wa miaka minne baada ya kumhadaa na kumlewesha bia.
Akisoma hukumu hiyo juzi, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Chiganga Tengwa alisema ameridhishwa na ushahidi pasipo kutia shaka uliotolewa mahakamani hapo na upande zote mbili za mashitaka na utetezi.



“Nimelazimika kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa baada ya mahakama hii kumtia hatiani ili iwe fundisho si kwake tu, lakini pia kwa wengine wenye tabia kama yako .... kitendo ulichomtendea mtoto huyo ni cha kinyama hustahili kuonewa huruma, “ alisema Tengwa.

Awali Mwendesha Mashitaka, Mkaguzi wa Polisi, Lazaro Masembo alidai mahakamani hapo kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Aprili 2 mwaka huu nyumbani kwa wazazi wa mtoto huyo ambako mtuhumiwa alikuwa ameajiriwa na wazazi wake kama mfanyakazi wa ndani.

Ilidawa mahakamani hapo kuwa siku hiyo ya tukio mama mzazi wa mtoto huyo alikuwa amekwenda kijiji cha jirani kutembelea ndugu zake ambapo alimwacha mtoto wake huyo chini ya uangalizi wa mshitakiwa.


Pia nyumbani hapo ilidaiwa mahakamani hapo kuwa kulikuwa na msichana aitwaye Nyasolo Doya (18 ) ambaye alikuwa mgeni wa nyumba hiyo ambaye alifikia hapo kujifungua.

Kwa mujibu wa Mwendesha Mashtaka, Masembo, mtuhumiwa alimwita mtoto huyo sebuleni ambako alikuwa amekaa na kisha akaanza kunywesha bia aina ya Balimi kisha akamlawiti huku mtoto akipiga kelele kwa maumivu akisikika akisema, “mama nakufa.”

Mahakama hiyo ilielezwa kuwa kufuatia kelele za kilio cha mtoto huyo, msichana Nyasolo Doyo alishtuka na kulazimika kukimbilia sebuleni ndipo alipomshuhudia mshitakiwa akimwingilia mtoto huyo huku akiwa amevua nguo zake.


Mwendesha Mashtaka Masembo alisema Nyasolo alipomsihi Baraka amwachie mtoto huyo aligeuka ‘mbogo' na kumtishia kuwa iwapo atatoa siri hiyo kwa wazazi wa mtoto huyo atamuua, ndipo msichana huyo aliponywea kwa hofu ya tishio hilo la kuuawa. 

Mahakama hiyo ilizidi kufahamishwa kuwa mama mzazi wa mtoto huyo alirejea nyumbani kwake saa mbili usiku na ndipo alipomwona binti yake huyo akitembea kwa kuchechemea mwendo uliomshtua mama huyo na akaamua kumuuliza msichana Nyasolo ambaye alimsimulia mkasa wote huo wa kusikitisha.



Mwendesha Mashtaka alidai mahakamani hapo kuwa mama huyo alilazimika kumpigia simu baba mdogo wa mtoto huyo ambae anaishi kijiji cha jirani ambae alifika nyumbani hapo saa nane usiku na ndipo walipoamua kumfungia mtuhumiwa mlango wa chumba chake kwa nje na kisha walienda kutoa taarifa kwa uongozi wa kijiji.


Katika shauri hilo upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi watano mmojawapo akiwa daktari aliyemfanyia uchunguzi wa kitabibu mtoto huyo na kuthibitisha kuwa alikuwa ameingiliwa na mwanaume katika sehemu zake za siri ambapo mshitakiwa hakuwa na shahidi yeyote.

Katika utetezi wake, mshitakiwa aliiomba mahakama imwachie huru kwa kile alichokieleza kuwa alisingiziwa tu.
CHANZO: VIJIMAMBO

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...