Thursday 18 July 2013

HAUSIGELI ANASWA AKIUZA FAMASI...KWA HALI HII TUTAPONA KWELI?

Stori: Chande Abdallah
OPARESHENI Fichua Maovu (OFM) chini ya Global Publishers bado ipo mzigoni ambapo wiki hii imenasa tukio la hatari baada ya kumbamba hausigeli akiuza duka la dawa muhimu ‘famasi’.
Hausigeli aitwaye Furaha akiwa dukani kama alivyonaswa na kamera za GPL.
Kamera za OFM zilitegwa baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa watu mbalimbali wakidai mhusika mwenyewe akiwa katika kazi nyingine tofauti na duka hilo.
Tukio hilo linadaiwa kufanyika kwa muda mrefu katika duka hilo lililopo Goroka, Toangoma, Kongowe, Temeke nje kidogo ya Jiji la Dar.


...Akiwa katika famasi akisubiri wateja.
Baada ya OFM kupokea taarifa hizo, ilianza utafiti wake ambapo iligundua kuwa mmiliki wa duka hilo anatambulika kwa jina la mama Atu.
Ikadaiwa kuwa mmiliki huyo ana tabia ya kumuachia duka hilo hausigeli wake aitwaye Furaha ili auze dawa kwa kubahatisha na mara kadhaa wagonjwa hupewa dozi ndivyo sivyo.
“Kuna mwenzetu alikuwa akiugua ugonjwa mwingine,  alipofika pale aliandikiwa dawa za malaria, hali yake ikawa mbaya hadi akakimbizwa hospitalini kulazwa, tulipomuonya mmiliki hakutusikia,” alisema mmoja wa watu wanaoijua ishu hiyo kiundani.
Ili kupata ushahidi kamili, OFM ilijifanya mgonjwa na kwenda kwenye famasi hiyo kuomba ushauri wa matibabu.
...Akimsikiliza mteja.
Hausigeli huyo alimtajia dawa za typhoid lakini shushushu wetu alimkwepesha na kumuomba chloroquine ambapo hausigeli huyo alikubali na kutaka kumpa bila wasiwasi.
Baada ya kushuhudia hayo OFM ilimfuata mwenyekiti wa mtaa huo, Issa Shomari kupitia mjumbe wake na kufika katika famasi hiyo  kujionea hali halisi ambapo kama ilivyokuwa mwanzo hausigeli huyo alikuwa tayari kutoa huduma.
Baada ya kikosi kazi kujitambulisha na kumhoji, alikiri kuwa yeye ni mtumishi wa ndani,  ana miaka 16, elimu ya darasa la saba, mwenyeji wa Iringa, huwa anaachiwa auze na mwajiri wake huku akifunguka kuwa hutoa dawa za malaria na magonjwa anayoyafahamu.
Akizungumza kwa mshtuko baada ya kujionea hali halisi, mwenyekiti huyo wa mtaa alisema kuwa atahakikisha anawasiliana na kamati ya afya ya Wilaya ya Temeke, Dar ili kuziondoa famasi kama hizo mtaani kwake.

CHANZO: GPL
Habari hii imenitisha sana wadau.Hivi watu wamekuwa na wanyama kiasi hiki?Mtu anathamini kipato zaidi ya uhai wa wengine?Nadhani imefikia wakati tuwe na sheria kali kwa watu wanaohatarisha uhai/maisha ya wengine.Hawa ni sawa na wauwaji tu.Hivi leseni za maduka haya zinatolewaje?Yaani ninajiuliza maswali mengi ambayo sina majibu.

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...