Wednesday 31 July 2013

MKOA KWA MKOA: LEO TUPO SONGEA MKOANI RUVUMA

Unapozungumzia historia ya Tanzania basi hutaacha kuitaja Songea,ambayo ni makao makuu ya mkoa wa Ruvuma. Songea ndiyo ilikuwa makao makuu ya vita vya majimaji vilivopiganwa kati ya mwaka 1905-1907. Jina la Songea linatokana na kionozi wa Wangoni aliejulikana kwa jina la Songea Mbano. Songea pamoja na viongozi wengine wa Wangoni,walinyongwa na Wajerumani mwaka 1906.
Mbali ya kuwa mkoa wa Ruvuma ni maarufu kwa kilimo hususan mahindi,vilevile kuna utajiri wa mawe a vito aina ya sapphire na ruby.Kwa kumbukumbu zangu binafsi uchimbaji huu umeshamiri katika wilaya ya Tunduru.


Hii ni barabara ya kuelekea Songea




Kanisa la Katoliki,Peramiho


Soko kuu la Songea
Baadhi a mitaa ya Songea mjini



Kaburi la halaiki walipozikwa mashujaa wa vita vya majimaji



Kaburi la Songea Mbano ambaye alizikwa peke yake na jina la mji wa Songea limetokana na jina lake


Mawe aina ya sapphire yanapatikana Songea


Mawe aina ya ruby yanapatikana Songea vilevile

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...