Friday 19 July 2013

NMB YAFADHILI SEMINA YA MAAFISA MAENDELEO WA VIJANA NCHINI

Benki ya NMB imefadhili semina kubwa iliyohusisha maafisa maendeleo wa vijana kutoka nchi nzima.Semina hii ambayo ilikua ni ya siku mbili ilifanyika katika kumbi za uwanja wa Taifa  jijini Dar es salaam. Mhe. Dkt.Fenera Mukangara ambae ni Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo alizindua rasmi semina hii na kuishukuru Benki ya NMB kwa ufadhili mkubwa ambao wamejitolea ili kufanikisha semina. Dhumuni la semina ni  kujadili maendeleo ya vijana kuanzia ngazi ya halmashauri,kuimarisha utendaji kazi kwa vijana wa mikoa na wilaya.
1Mhe. Dkt. Fenera Mukangara ambaye ni Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo  akiongea na maafisa maendeleo ya vijana nchini wakati wa uzinduzi wa semina ya siku mbili
2Katibu Mkuu Wizara ya Habari ,Vijana,Utamaduni na Michezo  Bw. Seth Kamuhanda akifafanua  jambo wakati wa semina hiyo.3Meneja wa NMB Mikopo Midogo Midogo Bw. Mashaga Changarawe akielezea huduma mbali mbali  zitolewazo na Benki ya NMB zikiwemo akaunti pamoja na mikopo mbalimbali kwa wajasiliamali
4Meneja Mawasiliano  wa NMB, Josephine Kulwa akizungumzia jinsi ambavyo Benki ya NMB kwa kupitia huduma zake kwa wajasiliamali inavyosaidia kuongeza ajira kwa vijana nchini
5Sehemu ya washiriki wa semina hiyo.
6Erick Shigongo naye alitoa maada kuhusiana  mafanikio na kujitambua katika ajira

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...