Monday 22 July 2013

Philippe aapishwa rasmi kuwa mfalme mpya wa Ubelgiji.

PHILIPPE
Mtoto wa Mfalme wa Ubelgiji Philippe ameapishwa kuwa mfalme wa saba wa nchi hiyo katika sherehe zilizofanyika kwenye bunge.
Mfalme Philippe mwenye umri wa miaka 53, amechukua nafasi hiyo kutoka kwa baba yake Mfalme Albert II, aliyetangaza kuachia madaraka hayo wiki tatu zilizopita kutokana na sababu za kiafya na umri.


Mfalme Albert II amekuwa mfalme wa Ubelgiji kwa takriban miaka 20.
Mfalme Albert amesisitiza nia yake kutaka kuiona Ubelgiji ambayo imegawanyika kati ya Wabelgiji wa kaskazini wanaozungumza Kiholanzi na Wabelgiji wa kusini wanaozungumza Kifaransa, wakiungana.
Mzozo huo kati ya pande hizo mbili, umesababisha kutokuwa na hali ya utulivu kisiasa nchini Ubelgiji kwa kipindi kilichopita.
Kazi kubwa za Mfalme Philippe ni kujaribu kutatua mzozo wa kikatiba wa nchi hiyo.
CHANZO: Mo blog

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...