Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Bi.Rukia Mtingwa(katikati)akiongea na baadhi ya kinamama wajasiriamali wadogowadogo wanaofanya biashara katika soko la Temeke Sterio jijini Dar es Salaam wakati walipofika sokoni hapo kutoa mikopo isiyokuwa na riba kwa kinamama hao kupitia mradi wa MWEI.
Meneja wa Vodacom Foundation kupitia mradi wa MWEI, Grace Lyon, akiwahakiki baadhi ya kinamama wajasiriamali wadogowadogo wanaofanya biashara katika soko la Temeke Sterio jijini Dar es Salaam wakati walipofika sokoni hapo kutoa mikopo isiyokuwa na riba kwa kinamama hao kupitia mradi wa MWEI wakati walipokuwawakikabidhiwa fedha zao za mikopo hiyo.
Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa( kulia) akishuhudia Karunde Mussa wa Kikundi cha uuzaji wa Mbogamboga katika Soko la Temeke Sterio jijini Dar es Salaam, akihesabu fedha kiasi cha shilingi Lakimoja baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa kikundi hicho Bi,Nikufya Mbengomwanja( katikati) wakati walipofika sokoni hapo kutoa mikopo isiyokuwa na riba kwa kinamama hao kupitia mradi wa MWEI.wakati walipokuwawakikabidhiwa fedha zao za mikopo hiyo.
Wanawake 400 katika wilaya ya Temeke wamenufaika na mikopo isiyokuwa na riba,Hii ni katika utekelezaji wake wa azima ya kampuni ya mawasiliano ya Vodacom kubadili maisha ya wanawake kwa kuwawezesha kukuza mitaji ya biashara na kuongeza kipato katika familia,kampuni hiyo imepanua wigo wa mpango wake wa kusaidia wanawake wanaojishughulisha na biashara ndogondogo - MWEI ambapo sasa inawafikia wanawake hata wa mijini.
Meneja wa mpango huo uitwao MWEI Grace Lyon ameyasema hayo wakati wa zoezi la kuwapatia mikopo nafuu isiyo na riba wala dhamana wanawake wajasiriamali zaidi ya 400 wa Wilayani temeke Jijijini Dar es salaam
Lyona emesema baada ya mpango huo kuleta mafanikio makubwa kwa wanawake wa vijijini pamoja an kuwepo kwa maombi ya kuwafikia wanawake wa mijini kampuni ya Vodacom imekubaliana na mawazo hayo na kwmaba ni Imani yake kuwa wanawake wa mijini watajiweka tayari kutumia fursa ya mikopo ya Mwei kujiinua kiuchumi.
"Kwa zaidi ya miaka mitatu minne sasa Mwei imekuwa ikielekeza Nguvu zake vijijini ambako tayari tumewafikia wanawake wengi katika mikoa mbalimbali, sasa tumeona ni vema mafanikio yale yawafikie na wanawake wa mijini ambao nao kimsingi wanahitaji kujengewa uwezo wa kumudu maisha."Alisema Lyon.
Kuhusu utekelezaji wa azima hiyo, Lyon amesema wameanza na Temeke lakini mipango ni kuzifikia wilaya nyengine za jiji la Dar es salaam huku akiwasihi wanawake hao kutambua kuwa hakuna kikubwa kilichooanza na kingi bali siku zote kikubwa huanza na kidogo
Amesema mafanikio makubwa ambyao wanawake wa vijijini wameyapata kupitia Mwei ni matokeo ya kujituma kwao, kuamini katika kidogo kufikia kikubwa na uaminifu katika urejeshaji w amikopo hiyo jambo ambalo limesaidia kuwafikia wanawake wengi zaidi ndani ya muda mfupi.
"Tunatambua kwua mazingira na hali ya maisha hayafanani kati ya mijini na vijijini unaweza kudhani kuwa mijini kuna changamoto nyingi za kibishara kuliko vijijini lakini nataka kuwaeleza kuwa kwa uzoefu nilionao wa kuwafikia wanawake wa vijijini kila mahali kuna changamoto zake kikubwa ni kuthamini kilicho mbele yako na kutumia ipasavyo kila fusra inayojitokeza.Aliongeza Lyon
Mradi huo wa Mwei amabo hutumia teknolojia ay mpesa kuwawezesah wakopaji kufanya marajesho kwa njia ya huduma hiyo jamabo ambalo linafanya gharama za ukopaji na urejeshaji w amikopo kuwa za chini zaidi kwa mkopaji.
Kwa upande wao baadhi ya wafanyabiashara hao wa Temeke wameelezea kufurahishwa na mpango hao hasa katika kipengele cha kutokuwepo kwa riba katika mikopo hiyo.
Kwa kweli tumekuwa na changamoto ya kupata mikopo lakini hata fursa za ukopeshaji zilizopo zinatukwaza na uwepo wa viwango vya juu vya riba, hapa tunapata kwa gharama nafuu na tunarudisha mkopo bila riba, tunashukuru kwa hilo."Alisema Mfanyabiashara wa Duka katika Soko hilo Tausi Mjape.
Aidha Nuru Njovu ambaye ni mfanyabiashara wa vitunguu katika soko hilo kwa upande wake ameshauri Vodacom kuwafikia wanawake wengi zaidi kwani itawakomboa wanawake katika lindi la umasikini.
CHANZO: Michuzi
CHANZO: Michuzi
No comments:
Post a Comment