Wengi tunapojenga numba zetu huwa tunasahau kuweka baadhi ya vitu muhimu nje ya nyumba zetu,hususan zile ambazo zina maeneo ya kutosha.Moja wapo ya vitu hivyo ni jiko la kuchomea nyama.Kuna aina mbalimbali za majiko ya kuchomea nyama kama yanayotumia nishati ya mkaa,gesi,umeme n.k.
Nitawaletea aina mbalimbali za majiko yanayotumia nishati mbalimbali, kwa kuanzia leo tunaanza na majiko ya kuchomea nyama yanayotumia nishati ya mkaa.Majiko haya ni rahisi kujenga na mtu yeyote anaweza kujenga nje ya nyumba yake kama anahitaji.
Zifuatazo ni baadhi ya picha za majiko hayo:
Nitawaletea aina nyingine za majiko haya ya kuchomea nyama hivyo endelea kutembelea blog yangu ili uweze kufanya uchaguzi ni jiko lipi linafaa nyumbani kwako.
No comments:
Post a Comment