Mshiriki aliyetolewa Big Brother 2013 "The Chase" Jumapili iliyopita Ammy Nando akiwa na Mussa Hussein (katikati) na Wasiwasi Mwabulambo kwenye Jahazi hii leo. Kuelezea kulikoni mapaka nusura wazichape na Elikem.
Ammy Nando katika picha ya pamoja na Mtayarishaji wa kipindi cha Jahazi la Clouds FM Emmanuel Likuda. Nando alikua mualikwa kwenye kipindi hicho kwa ajili ya kuelezea kisa na mkasa ya kwanini alitaka kuzichapa na Elikem kwenye jumba la Big Brother 2013 "The Chase" ugomvi uliopelekea Nando kutupwa nje ya kinyang'anyiro hicho.
Nando akiwa na Dj Fetty wa Clouds FM
Nando ambaye aliondolewa wiki iliyopita kwa kuvunja miongoni mwa sheria za shindano hilo alikuwa akiongea leo kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM.
“I live my life with no regrets,”alisema Nando.
“Sitaki sijui matatizo wala nini, kilichotokea ndio kimetokea, najipanga upya naendelea na maisha mengine. Vingapi vimetokea vingine vizuri nyuma mpaka unapoenda vinakuja vizuri na vizuri kila siku? Tokea nilipotokea mimi nilipokuwa mtoto mdogo nani alikuwa ananijua? Sasa hivi nipo peace yaani, nashukuru kwamba mmenipokea vizuri. Naendelea na maisha, uzuri nimepata platform ya kutengezeza jina langu, kwahiyo naenda hivyo hivyo mpaka huko ntakapofika.”
SIKILIZA MWENYEWE MAHOJIANO:
No comments:
Post a Comment