Monday, 5 August 2013

Angalia picha za ujenzi wa barabara na vituo vya mabasi ya kasi Jangwani – Kimara, Dar es salaam








Kutokana na foleni kubwa ambayo imekuwa tatizo kwa wakazi wa Dar es salaam hasa wenye shughuli zinazowalazimu kufika mjini, serikali ilianzisha mradi wa mabasi yaendayo kasi ikiwa ni moja ya mipango ya kuepusha foleni.
Huu mradi umeanza na ujenzi ambao unaweza kuonekana hasa kwenye barabara ya Morogoro, hii hapa ni update jinsi mradi huo unavyoendelea hivi sasa kuanzia stendi kuu pale Jangwani hadi Kimara mwisho.

Ukifika Jangwani hii ndiyo view ya mjini kama unavyoona kwa mbali

Bango la ujenzi unakutana nalo ukiwa unaingia kwenye site ya kituo kikubwa

Muonekano wa mbele wa jengo la kituo kikubwa cha mabasi yaendayo kasi

.

Hapa ni ndani ya jengo na kutakuwa na migahawa na bar kwa ajili ya abiria kusubiria mabasi yafike
Ukiwa bar au restaurant, hii ndiyo view yako ambayo ni parking ya mabasi yenyewe ambapo basi likifika unaenda zako kupanda

Mabasi yatakuwa yanajipanga hapa

Pembeni ya jengo kuna ofisi na garage ya hayo mabasi

Ujenzi bado unaendelea na mashine zipo zinafanya kazi

Haya mabomba yanatumika kujenga mfumo mzuri wa maji taka kwasababu mitaro mingi imefukiwa ili barabara ijengwe.

Ilikuwa ni jumapili lakini kazi  inaendelea kama kawaida

Ukitoka Jangwani ukafika mbele kidogo Magomeni Usalama kituo kimeshawekwa hadi kibao cha utambulisho.

Mtu wangu wa nguvu hapohapo Magomeni pia kuna tawi la NMB Bank, unaweza kufika na kujipatia huduma za kibenki pia.

Vituo vya haya mabasi ni virefu kama unavyoona mwenyewe ambapo basi litakua linapaki kwa pembeni alafu ndani ya hizo chuma ndio kutakua na viti na vioo kwa ajili ya abiria kupumzika na kusubiri basi.

Safari ilifika Manzese, huu ni muonekano wa maendeleo ya barabara kutoka kwenye daraja la Manzese na kituo kinaonekana kwa mbali.

Upande wa pili wa daraja la Manzese na barabara inaonekana kuendelea vizuri
OLYMPUS DIGITAL CAMERA

Haya magari yanafanya kazi za mfumo wa maji taka pembeni ya daraja la Manzese

Ukiwa kwenye lile daraja unaweza pia kuliona jengo la Milleniums tower kwa mbali.
OLYMPUS DIGITAL CAMERA

Safari ikafika Ubungo, kuna vitu vinafanyika kwenye huu ujenzi kwa mtu ambaye sio mtaalamu au haujaiona ramani ya ujenzi huu sio rahiis kuelewa ni nini wanafanya, mfano hapa sikupata hata mwenyeji wa kunielezea ni kitu gani hiki.

Ubungo stand ya mkoa hapo.

Bado tupo Ubungo

Hiki ni kitu kama daraja kinajengwa na mara ya mwisho napita hapa halikuwepo, leo nimeona mabadiliko.

Upande huu unaungana na stendi ya mkoa.

Ukitoka Ubungo, ujenzi mwingine utaukuta Kimara ambapo kuna kituo kikubwa sana kinajengwa
OLYMPUS DIGITAL CAMERA
OLYMPUS DIGITAL CAMERAOLYMPUS DIGITAL CAMERA
OLYMPUS DIGITAL CAMERA
OLYMPUS DIGITAL CAMERA
CHANZO:Millard Ayo

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...