Na Gladness Mallya
MWANAMUZIKI wa Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’ amefunguka kuwa kwa sasa haielewi afya yake kwani kila kukicha anajihisi hayuko sawa.

Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Banza alisema kuwa anahisi mabadiliko na amepoteza hata hamu ya kula, hali inayosababisha mwili wake upungue na kushindwa hata kufunga.
“Naamini Mungu anaona matatizo yangu, namuomba anisamehe kwa sababu siwezi kufunga kutokana na afya yangu kutokuwa nzuri. Siku za hivi karibuni nimepoteza hamu ya kula kabisa, kula kwangu ni kwa shida,” alisema Banza bila kuweka wazi tatizo linalomsumbua.

CHANZO: GPL
No comments:
Post a Comment