Wednesday 21 August 2013

KIZIMBANI KWA KUKUTWA NA `UNGA`


Edson Monyo

Mfanyabiashara Edson Monyo (39) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, akikabiliwa na mashitaka  mawili ikiwamo kukutwa na dawa za kulevya zenye thamani ya Sh. milioni 68.

Mshtakiwa huyo alisomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Hellen Riwa.

Wakili wa serikali Leonard Challo alidai kuwa Agosti 4, mwaka huu katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere alikamatwa na askari  akiingiza kilo 1,512.69 za dawa za kulevya aina   ya Heroin Hydrochloride zenye thamani ya Sh. 68,069,250.

Katika shtaka la pili ilidaiwa kuwa siku na tarehe ya tukio la kwanza mshtakiwa alikamatwa na askari akiingiza nchini dawa za kulevya aina ya bangi  yenye uzito wa gramu 34.77 yenye thamani ya Sh.13, 908,000.

Wakili Challo alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Hata hivyo, Hakimu Riwa alisema mshitakiwa hatakiwi kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi ya dawa zenye thamani zaidi ya Sh. milioni 10.

Aidha, kesi hiyo upelelezi wake utakapokamilika itasikilizwa Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam.

Mshitakiwa alikana shtaka la pili la kukamatwa akiingiza bangi nchini.
Hakimu Riwa alisema mshitakiwa apelekwe mahabusu hadi Septemba 3, mwaka huu, kesi hiyo itakapotajwa.
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...