Tuesday, 20 August 2013

Mwakyembe apongezwa kwa kuwaumbua maofisa JNIA


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Baraza la viongozi wa dini kupambana na dawa za kulevya nchini, Sheikh Alhad Mussa Salum

Uthubutu wa Waziri wa Uchunguzi Dk. Harrison Mwakyembe kwa kupambana na mtandao wa dawa za kulevya na kuiomba serikali kumuongezea ulinzi, umepongezwa na viongozi wote wa dini nchini.



Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Baraza la viongozi wa dini kupambana na dawa za kulevya nchini, Sheikh Alhad Mussa Salum, alisema wanampongeza waziri kwa uzalendo, ujasiri, upendo na huruma kwa Taifa.

Mussa ambaye ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, alisema Dk. Mwakyembe ni mfano wa kuigwa kwa viongozi wote nchini, hivyo baraza linawaomba viongozi wote wa dini kumwombea kwa kuwa uthubutu wake ni hatari kama asipopewa ushirikiano.

"Dk. Mwakyembe amerejesha heshima uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere ni hatua muhimu sana, heshima kwa nchi na tusikubali uwanja huo kuwa  ndiyo njia kuu kupitisha dawa haramu za kulevya," alisema.

Wiki iliyopita, Waziri Mwakyembe aliwataja maofisa waliohusika kuruhusu dawa za kulevya kupitishwa kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), ambao ni Yusufu Daniel Issa, Jackson Manyonyi, Juliana Thadei na Mohamed Kalungwana na kuamuru wafukuzwe kazi   na wafunguliwe mashitaka ya jinai.
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...