Mmoja wa watoto wanaendelea na matibabu Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam, akiwa bize na rangi wakati walipotembelewa na mchora katuni Nathan Mpangala kupitia mradi wake wa kujitolea wa Wafanye Watabasamu, Jumamosi iliyopita. Mradi huo unaoshirikisha ndugu, jamaa, marafiki na wachoraji wenzake, ulikwenda kuwafariji kwa kuwapa zawadi kisha kuchora nao.
Mratibu wa mradi wa kujitolea wa Wafanye Watabasamu, Katunisti Nathan Mpangala ‘Mtukwao’, akishea jambo na mmoja wa malaika Hospitali ya Taifa Muhimbili, upande wa saratani, Jumammosi iliyopita.
Sanaa inamchango mkubwa katika kupunguza msongo wa mawazo na kusahaulisha maumivu.
Mchora vibonzo wa ITV ambaye pia ni mratibu wa Wafanye Watabasamu, Nathan Mpangala akiwa na mchora vibonzo wa baadae.
NYUMBA TU, SIMPO. Akiendelezwa atakuja kuwa mchoraji mahiri wa majengo.
Mchoraji katuni wa gazeti la Nipashe, Abdul King O aka ‘Kaboka mchizi’, aliungana na Wafanye Watabasamu kuwatabasamisha malaika hawa.
KUCHORA TU, HAPA MMEFIKA! Pamoja na maumivu ya saratani aliyonayo, bado aliweza kuthibitisha kuwa anaweza.
HEBU NIJIACHIE MIE. Ama hakika linapokuja suala la kuchora, hakuna mtoto anayekataa.
NYUMBA TU, SIMPO. Akiendelezwa atakuja kuwa mchoraji mahiri wa majengo.
Mchora katuni Adam Lutta aka Baba Tau, alikuwa miongoni mwa Wana-Wafanye Watabasamu.
KAZI IMETULIA
CHANZO: Hathan Mpangala
No comments:
Post a Comment