Thursday, 8 August 2013

NMB YAZINDUA ASASI YA MAENDELEO YA KILIMO (NMB FOUNDATION FOR AGRICULTURAL DEVELOPMENT)

Mwanzoni mwa wiki Benki ya NMB ilizindua taasisi ya maendeleo ya Kilimo nchini Tanzania.Taasisi ambayo inakusudi la kuinua sekta ya kilimo kwa kuanzia ngazi ndogo kabisa inayomgusa mkulima mdogo hadi ngazi ya wakulima wakubwa na kilimo cha biashara.Wakulima wadogo wadogo wamekua hawatambuliki kutokana na kutokua na mtaji wa kutosha na uwezeshwaji kutokuwepo.Hivyo Benki ya NMB kwa kupitia taasisi hii itawasaidia wakulima kwa kupitia vyama au vikundi ili kuwezeshwa katika uzalishaji na kuinua sekta nzima ya kilimo.
4Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji Dk. Mary Nagu akisalimiana na baadhi ya wadau wa kilimo waliohudhuria uzinduzi wa Taasisi ya Maendeleo ya Kilimo ya Benki ya NMB mjini Dodoma. Nyuma ya Waziri Nagu ni Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Mark Wiessing. 
2Mkuu wa Shughuli za Kilimo wa Benki ya NMB, Robert Pascal akitoa maelezo juu ya Taasisi hiyo namna itakavyofanya kazi na kua msaada mkubwa kwa wakulima kabla ya uzinduzi uliohudhuriwa na baadhi ya wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakulima na wadau wa kilimo. 
3Baadhi ya wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya mbalimbali mbali nchini na wadau wa Kilimo wakifuatilia Hotuba ya Afisa Mtedaji Mkuu wa Benki ya NMB, Mark Wiessing (kulia)

4 (1)Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya NMB, Prof. Joseph Semboja akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji Dk. Mary Nagu (katikati) baada ya kuzindua taasisi ya Maendeleo ya Kilimo ya Benki ya NMB mjini Dodoma . Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi,C.E.O wa NMB, Mark Wiessing na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo ya Kilimo ya Benki ya NMB, Vallerian Fernandos

5Meneja Mawasiliano  wa Benki ya NMB,Josephine Kulwa akimsikiliza kwa makini Mhe. Dk. Mary Nagu kabla ya hafla ya uzinduzi kuanza kati kati ni Meneja wa NMB kanda ya Kati Ole Loibanguti.

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...