Friday 30 August 2013

NZOWA ATISHIWA KUUAWA!

Makongoro Oging' na Haruni Sanchawa
VITA kupinga madawa ya kulevya imeingia katika hatua nyingine, safari hii Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa amejikuta katika wakati wa hatari baada ya kutumiwa meseji za vitisho kwa maisha yake.


Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa.
Habari za uhakika zinadai kuwa, tangu vita hiyo ipambe moto, baadhi ya watu wanaodaiwa ni vigogo wa biashara hiyo haramu wamekuwa wakimtumia ujumbe mfupi wa maneno (SMS) wakisema ajiangalie wanaweza kumtoa uhai.
Kwa mujibu wa mnyetishaji wetu, watu hao wengine wanasema watatumia risasi kumtoa uhai huku wengine wakidai watamchoma moto bila kufafanua ni moto upi.
Taarifa nyingine za ndani zaidi zinadai kwamba, maisha ya Kamanda Nzowa kwa sasa ni kama digidigi kwa vile anaishi kwa kujificha ili kukwepa kuonekana kwenye hadhara lengo ni kukwepa kufanyiwa kitu mbaya.
Kuhusu wabunge kudaiwa kutajwa kwa wingi kwenye makundi ya wauza unga, habari zinasema ndani ya moyo wa Nzowa ndiko kwenye majina hayo.
“Nataka kusema jambo moja, wabunge kweli wanatajwatajwa sana kujihusisha na madawa ya kulevya, lakini nataka kukwambia kuwa Nzowa ana siri nzito,” kilisema chanzo hicho.
Kilisema kuwa, ni yeye ndiye mwenye hayo majina na atakayeyapeleka kwa wakubwa wake serikalini, hivyo iko sababu ya serikali kuhakikisha maisha ya mzee huyo yanalindwa kama ya viongozi wengine wa kitaifa.
Agosti 28, mwaka huu, Ijumaa lilimtafuta Kamanda Nzowa na kufanikiwa kukutana naye uso kwa uso ofisini kwake, alipoulizwa kuhusu kutishiwa maisha alikiri.
“Ni kweli, nimekuwa nikitumiwa meseji za vitisho kila mmoja akisema lake. Wengine wanasema wataniua kwa risasi, wengine kwa moto sijui.
“Ni mambo mengi ziwezi kuyasema kwani siogopi mtu, mimi naitumikia nchi yangu. Wewe si unaona siku hizi, unadhani mtu anaweza kutembea na madawa ya kulevya kifua mbele kama zamani?” alihoji Kamanda Nzowa.
Ijumaa: Lakini kamanda unapata ulinzi wa kutosha? Maana kwa hii shughuli yako unatakiwa kulindwa sana.
Nzowa: Ulinzi ni wa kawaida, lakini sehemu kubwa ya maisha yangu ulinzi namwachia Mungu kwa sababu anasema yeye asipoulinda mji waulindao wakesha bure.
Kamanda Nzowa alikwenda mbele zaidi kwa kuwaonesha mapaparazi wetu maandiko kwenye Kitabu Kitakatifu cha Biblia Agano la Kale katika Zaburi ambapo kunazungumzia mtu awe anamtumaini Mungu katika ulinzi.
CHANZO: GPL

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...