Sunday 25 August 2013

Orodha ya majina ya waliochaguliwa kufanya usaili wa kujiunga na Jeshi la Polisi



Jeshi la Polisi Tanzania limetoa majina na ratiba ya usaili kwa vijana waliomaliza kidato cha nne mwaka 2012 na waliomaliza kidato cha sita mwaka 2013 ambao wamechaguliwa kufanya usaili kabla ya  kujiunga na Jeshi la Polisi.

Muhimu:

  • Mwombaji anaruhusiwa kufanya usaili kwenye kituo chochote cha usaili kilicho karibu naye kulingana na tarehe zinavyoonesha kwenye jedwali hapo  juu ili mradi tu awe amejiridhisha kuwa ni miongoni mwa walioitwa kwenye usaili. Jeshi la Polisi halitahusika na lawama yoyote ile kwa mtu atakayekwenda kwenye kituo cha usaili hali ambapo jina lake si miongoni mwa walioitwa kufanya usaili.
  • Mwombaji aliyeitwa kwenye usaili aje na vyeti vyake vyote vya masomo [(Academic Certificate(s)/Results slip(s) & Leaving certificate(s)], nakala halisi ya cheti cha kuzaliwa (Original Birth certificate). Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika.
  • Mwombaji  awe na namba ya simu itakayotumika kumjulisha endapo atachaguliwa..
  • Kila mwombaji aliyeitwa kwenye usaili atajigharamia usafiri, chakula na malazi kwa muda wote wa zoezi la usaili. Pia waombaji waje na kalamu za wino kwa ajili ya usaili wa kuandika.

Ni muhimu sana kwa kila mwombaji kuzingatia muda wa kuanza usaili.




No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...