JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA UCHUKUZI
MAMLAKA YA HALI YA HEWA
Simu: +255 22 2460706-8...
WIZARA YA UCHUKUZI
MAMLAKA YA HALI YA HEWA
Simu: +255 22 2460706-8...
Telefax: +255 22 2460735, 2460700 S.L.P. 3056,
Barua pepe: met@meteo.go.tz DAR ES SALAAM
Tovuti: www.meteo.go.tz
Unapojibu Tafadhali nakili:
Kumb. No.TMA/4060/6/7: 20 Agosti 2013
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Serikali yaanza kutoa masomo ya elimu ya juu ya sayansi ya hali ya hewa nchini.
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania kimefanikisha uanzishwaji wa masomo ya shahada ya kwanza ya sayansi ya hali ya hewa (Bsc. Meteorology) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kuanzia muhula wa masomo 2013/14.
Mchango wa Mamlaka katika kufanikisha uanzishwaji wa hiyo pamoja na kushiriki katika kuandaa mitaala ya kufundishia, kuhakikisha Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) linatambua uanzishwaji wa shahada hiyo, kutoa wataalamu wa kufundisha kozi mbalimbali na kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya mafunzo ya vitendo kwa wanachuo.
Kuanzishwa kwa mafunzo hayo hapa nchini, ni moja ya utekelezaji wa agizo la Mheshimiwa Rais, pia kutatoa fursa kwa idadi kubwa ya watanzania, wageni kutoka nje ya nchi, na watumishi wa Mamlaka kwa ujumla kujiunga na masomo hayo ya juu katika taaluma ya hali ya hewa kwa gharama nafuu.
Kwa upande wa Mamlaka, mafunzo hayo yatasaidia kuokoa gharama kubwa iliyokuwa ikitumika kusomesha wataalamu wa hali ya hewa nje ya nchi. Aidha itasaidia kuongeza idadi ya wataalum wakutosha ikizingatiwa hivi sasa gharama yake itakuwa ndogo kulinganisha na hapo awali.
IMETOLEWA NA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
No comments:
Post a Comment