Friday 16 August 2013

WAZIRI MWAKYEMBE ATEMA CHECHE

Waziri Mwakyembe akielezea jinsi madawa ya kulevya yanayopitishwa uwanja wa ndege jijini Dar.
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akiwasili ndani ya ukumbi kwa ajili ya kuongea na wanahabari.
Waandishi wa habari wakiwa ndani ya ukumbi wakimsubiri Waziri Mwakyembe.
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harisson Mwakyembe ameng'aka na kueleza jinsi madawa ya kulevya yanavyopitishwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Waziri Mwakyembe ameelezea hayo leo wakati akiongea na wanahabari ofisini kwake na kutoa tamko la serikali kuhusu biashara hiyo haramu. Kufuatia matukio ya kukamatwa kwa dawa za kulevya katika uwanja huo, serikali imewafukuza  kazi na itawafikisha mahakamani watumishi wake watano na askari polisi mmoja wa uwanjani ambapo maofisa wa usalama wa taifa waliochelewesha kuwapeleka mbwa uwanjani hapo siku ya tarehe 05 Julai, 2013 na kupitisha kiasi kibubwa cha dawa za kulevya wanachunguzwa.
(PICHA NA HABARI, SANCHAWA / GPL)

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...