Tuesday 20 August 2013

Zari kurejesha kipindi chake




Baada ya awamu ya kwanza ya kipindi chake cha Televisheni cha Maisha ya Uhalisia kusimamishwa, Nyota wa nchini Uganda, Zarina Hassan kwa sasa yupo katika maandalizi ya awamu nyingine ya kipindi hicho ambayo itaanza kwenda hewani hivi karibuni.


Zari ameendelea kukifanyia kazi kipindi hiki akiwa karibu kabisa na Sylvia Owori, mwanadada ambaye kwa pamoja walisababisha kipindi cha kwanza kusimamishwa kutokana na kuonyesha mambo ambayo hayakuwa yakiakisi utamaduni wa Uganda.

Hatua ya Zari kukomaa kurudishia uhai kipindi chake tena inakuja sambamba na taarifa za Bobi Wine ambaye naye pia ana kipindi cha maisha ya uhalisia, kufanya mabadiliko makubwa kwenye kipindi chake ili kukiletea msisimko wa kipekee.
CHANZO: EATV

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...