Sunday, 1 September 2013

ANGALIA PICHA ZA IBADA YA KUUAGA MWILI WA ASKOFU KULOLA JIJINI DAR ES SALAAM

Picha wakati wa ibada ya heshima kwa mwili wa aliyekuwa askofu mkuu wa kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania(E.A.G.T) iliyofanyika katika kanisa hilo Temeke jijini Dar es salaam ambapo makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Mohamed Ghalib Bilal alikuwa miongoni mwa viongozi walioshiriki katika ibada hiyo.
Wabunge wa chama cha Mapinduzi mh. mchungaji Getruda Rwakatare pamoja na Asumpta Mshama wakitia saini kitabu cha wageni.




Askofu mkuu wa WAPO Mission International Sylvester Gamanywa akimfariji mke wa marehemu.
PICHA ZAIDI BOFYA READ MORE




Askofu mkuu wa kanisa la Ufufuo na uzima, Josephat Gwajima akitoa salamu zake " Shujaa amerejea nyumbani"
Mtume na nabii Anthony Lusekelo a.k.a Mzee wa Upako akizungumza.


Mheshimiwa Philip Mangula akizungumza mengi kuhusu walivyofahamiana na marehemu, aliwagusa wengi alipomalizia kwa kuimba pambio la iende mbele injili.




Mheshimiwa Mangula na mkewe wakitoa salamu zao za rambirambi kwa mke wa marehemu.





Mheshimiwa mbunge wa Nkenge mkoani Kagera na mchungaji msaidizi wa kanisa la Mito ya baraka ambaye pia ni mama mzazi wa waimbaji wa kundi la J'sisters akitoa salamu zake za rambirambi.
Mheshimiwa Dkt, mchungaji Getruda Rwakatare akitoa salamu zake.


Balozi na mkuu wa mkoa wa Dar mstaafu Mh. Mary Chipungahelo akitoa salamu.
Waziri Theresia Uvinza akizungumza. 


Meza kuu ilisheheni.


Askofu Zachary Kakobe akizungumza maneno yaliyowagusa wengi hasa ujumbe wake kwa kanisa la E.A.G.T pamoja  na mitume na manabii kuacha tamaa ya fedha.


Watoto, wajukuu na ndugu wakiwa katika huzuni.


Mtume Onesmo Ndegi wa Living water Makuti Kawe akitoa salamu.
Makamu wa Rais akitia saini kitabu cha maombolezo.
Mjane mama Moses Kulola akiwa mwenye huzuni kubwa.


Meza kuu.




Makamu wa Rais akitoa salamu na pole kwa wafiwa.
Mwimbaji wa injili Abihudi Misholi akiimba wimbo maalumu wa kumuaga askofu Kulola msibani hapo.




Katibu mkuu wa Chadema, Dkt Wilbroad Slaa akitia saini kitabu cha maombolezo.




Akizungumza na waombolezaji msibani hapo.


Makamu wa Rais wa aliyezibwa na mpiga picha akitoa heshima zake za mwisho.CHANCO: Gospel Kitaa

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...