Assalaam Alaykum.
Kufuatia kichwa cha habari kilichopo hapo juu, nachukua fursa hii kutoa Historia fupi ya Kijana huyu anako toka na jinsi ugonjwa alionao ulivyo gundulika mpaka hivi sasa.
Zuberi Mgeni Zuberi alizaliwa Mwaka 1995 katika Kijiji cha Kwale Kata ya Kwale Wilaya [mpya] ya Mkinga Mkoa wa Tanga. Alifanikiwa kumaliza Shule ya Msingi kwenye Kata yake hiyo na akabahatika kuchagulia Mwaka 2010 kuendelea na Masomo ya Sekondari ambayo ipo kwenye kata hiyo. Lakini hakuweza kuendelea na Masomo hayo kwa ajili ya Ugonjwa huo. Mwandishi wa habari hii ni Ndugu wa karibu wa Mama yake Zuberi.
Bado wanaishi pamoja na Baba mzazi wa Zuberi hadi leo na jina lake ndilo hilo Mgeni.
Shughuli wanazo fanya ni Uvuvi na Ukulima mdogo. Kipato chao ni cha hali ya chini kiasi walishindwa kumfanyia uchunguzi Kijana wao ili wafahamu ni kipi kinacho msumbua Mtoto huyo ambaye mara kwa mara alikuwa akisumbuliwa na Tumbo hivyo kufikiria kuwa ndiyo Maradhi yanayo msibu, kwahiyo walikuwa wa kimpatia Dawa za Tumbo ambazo hazikua zikitoa nafuu ya moja kwa moja na ilibidi awachishwe kundelea na Masomo ya Sekondari ndipo hapo Mwandishi wa Habari hii ambaye wakati huo alikuwa akiishi Kisiwani Pemba kwa shughuli za Ujenzi wa Barabara alipo fahamishwa na akatoa msaada wa ushauri na fedha ili Kijana apelekwe kwenye Hospitali ya Rufaa ya Bombo Mjini Tanga kwa Uchunguzi na tiba husika Mwaka 2011 Juni.
Hapo ndipo alipo gundulika kuwa anasumbuliwa na Ugonjwa ndani ya Moyo wake hivyo Hospitali hiyo ikampa Rufaa ya Kwenda Hospitali ya Taifa ya Mhimbili ambapo amekuwa na Kliniki hadi leo.
Cha kusikitisha ni kuwa Madaktari wa Hospitali hiyo wameshindwa kumpa Rufaa ya kwenda Nchi za nje kwa Matibabu kamili baada ya wao kutokuwa na vifaa au ujuzi wa Tiba hiyo, hivyo ilibidi kutafutwa njia nyengine kwenye Hospitali Binafsi ikiwemo Regency ambao baada ya utafiti wao wakasema anahitajika kwenda India kwa Matibabu na Gharama kwa kipindi hicho zilihitajika wastani wa Dola 6000 za Kimarikani sawa na Shs.9,600,000/= za Tanzania.
Zikipatikana anaweza kusafirishwa na Msaidizi wake mmoja. Maelezo Mengine kwa kina yana weza kupatikana kwa kuwasiliana na Mwandishi wa Habari hii [Mjomba] moja kwa moja kwa kutumia Nambari zifuatazo:- 0777 980492 au 0714 980492 Jina lake ni Bwana Yunus Ally Chui na Mshirika wake wa karibu ni Bwana Feisal Y. Chui Nambari yake ni 0773 449662.
Msaada wa ki Fedha unaweza kutumwa kwenye Akaunti zifuatazo: 5753735527 kwa Fedha za Kitanzania na 5753735502 kwa Fedha za Kigeni Bank ya Exim Tawi la Tanga kwa Jina la Yunus Ally Chui.
Ina ambatanishwa kwenye Barua hii Picha ya Zuberi ili kuthibitisha namna gani Ugonjwa huu ulivyo mbadili Umbile lake.
Ina ambatanishwa kwenye Barua hii Picha ya Zuberi ili kuthibitisha namna gani Ugonjwa huu ulivyo mbadili Umbile lake.
SHUKRAN
Yunus Chui.
CHANZO: Kapingaz
No comments:
Post a Comment