Wednesday 25 September 2013

KENYA YAOMBOLEZA KWA SIKU 3


Kenya inaanza siku tatu za maombolezi ya kitaifa kwa waathiriwa wa mashambulizi ya kigaidi yaliyofanyika katika jengo la kibiashara la Westgate mjini Nairobi.

Rais Uhuru Kenyatta pia ameseama kuwa bendera zitapepershwa nusu mlingoti kwa heshima ya waliopoteza maisha yao katika mashambulizi hayo.

Maafisa wa uchunguzi wa kimataifa wanaungana na wale wa Kenya kujaribu kuondoa mili ambayo imenaswa kwenye vifusi vya jengo hilo ambalo sehemu yake iliporomoka jana. Nia ni kujaribu pia kutambua uraia wa washambulizi hao.Watu 67 wameuawa ikiwemo wanajeshi kadhaa wa usalama, ingawa kuna hofu kuwa idadi ya waliofariki huenda ikaongezeka.

Baraza la usalama wa kitaifa linatarajiwa kukutana leo kudadisi yaliyotokea na kujiandaa kwa mkakati mpya wa kigaidi.


Magaidi watato wa kundi la Al Shabaa lililokiri kutekeleza mashambulizi hayo,waliuawa katika shambulizi hilo lililodumu siku nne na kuwa washukiwa wengine 11 walikamatwa wakijaribu kuondoka nchini.
Katika hotuba yake kwa taifa siku ya Jumatano , Rais Uhuru Kenyatta alisema kuwa alihisi uchungu mkubwa na kuwa Kenya imejeruhiwa vibaya,lakini alielezea matumaini kwa kuwa shambulizi limeisha na kusema kwamba waliohusika watakiona cha mtemakuni.
Wakati huohuo, afisaa mmoja mkuu wa serikali ya Somalia, amesema kuwa hakuna suluhu la kijeshi kwa kundi la wanamgambo wa Al Shabaab nchini humo. Wanamgambo hao wameitikia kuhusika na mashambulizi ya kigaidi nchini Kenya ambao watu zaidi ya sitini wameuawa.
Akizungumza na mjumbe wa nchi hiyo katika Umoja wa Mataifa, Yusuf Mohamed Ismail Bari Bari, alisema kuwa serikali yake na jamii ya kimataifa inapaswa, kungazia zaidi mizizi ya tatizo la magaidi hao, upatikanaji wa rasilimali pamoja na uwakilishi wa kisiasa.
CHANZO: BBC

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...